Somo la 1: Kwanini Tujifunze Biblia

Kozi ya Kujifunza Biblia

Somo la 1: Kwanini Tujifunze Biblia?

Mwandishi: Bob Thiel

Utangulizi: Kozi hii imetokana na kozi ya awaliiliyoitwa “Kozi ya Biblia kwa Mawasiliano” iliyoandaliwa mwaka 1954.  Iliyoanzishwa chini ya uangalizi wa marehemu C. Paul Meredith enzi za Radio Church of God. Vipengele kadhaa vimeboreshwa viendane na karne ya 21(japo mengi ya mafundisho ya awali hayakubadirishwa). Pia imeongezewa aya za Kimaandiko, pamoja na taarifa na maswali ambayo hayakuwemo kwenye kozi ya awali.

Kwa nini Tujifunze Biblia?

KWA NINI TUHITAJI kujifunza Biblia katika karne hii ya 21? Biblia ni nini?  Tunapaswa tujifunze namna gani, ili tuweze kuielewa? Katika mwanzo kabisa wa kozi hii tunahitaji kujiuliza maswali haya na kuyajibu.

Biblia inafundisha: “JIFUNZE KWA BIDII KUJIONYESHA KWA MUNGU KUWA UMEKUBALIWA NA YEYE” (2 Timotheo 2:15) and “Jifunze kutenda mema” (Isaya 1: 17). Hivyo, Wakristo wanapaswa kujifunza kwa kuwa Maandiko yamewaagiza hivyo.

LAKINI ni kwa nini tuhitaji kujifunza na kukubaliwa na Mungu? Na huku kujifunza kunahitaji kuwe ni WAJIBU wa kuchosha na usio wa kusisimua ambao tunajilazimisha kuufanya sababu ya kumtii mungu mkali-ama kujifunza huku kunatakiwa kuwe kwa KUBURUDISHA, kuwe kwa KUCHANGAMSHA na kwa KUFURAHIA kuletako FAIDA kuliko tulivyowahi kuona katika uhai wetu?

KWANINI kwa walio wengi kujifunza Biblia ni jukumu la kuchosha, lisilo na msisimko, lililojaa mateso-lifanywalo, kwa vile tu ni wajibu na kutokana na kumwogopa Mungu katili?

Ni kwa vile tu walio wengi HAWAJAMJUA Mungu, wala ni wa namna gani- na ni kwa sababu bado hawajaanza KUIELEWA Biblia kiukweli!

Kwanini tujifunze Biblia?

Ziko sababu nyingi.

Wanadamu bila ya Mungu wanajipeleka kwenye uangamizi wa sayari hii kwa vile wamejitenga na Muumba wao Mungu (Mathayo 24:22). Ni watu wachache tu wanalielewa hili kwa usahihi, na kile Mtume Petro alichosema, kwamba Yesu ndiye “aliye na maneno ya uzima wa milele” (Yohana 6:68).

Sehemu muhimu mbalimbali za Biblia ziliandikwa zikiwa na maneno yaliyotamkwa moja kwa moja na Yesu mwenyewe pale alipotembea hapa duniani akiwa katika mwili (Mfano: Mathayo, Marko, Luka, na Yohana), na maeneo mengine yaliandikwa ili tuweze kujua kile ambacho yeye alikifundisha na jinsi gani tunapaswa kuishi (mfano: 1 Wakorintho 1:11; Methali 1:1-7).

Fahamu pia:

“16 Kila andiko, lililovuviwa na Mungu lafaa kwa mafundisho, kwa kuwaonya watu makosa yao, kuwaongoza na kuwafundisha katika haki; 17 ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila kazi njema” (2 Timotheo 3:16-17).

Ikiwa kweli unahitaji kuwa mfuasi wa Yesu, na uwe umekamilika, unahitaji kujifunza na kuyapokea maelekezo, uwe tayari kusahihishwa, na kuonywa kutokana na kile Biblia ilichonacho.  Ukweli ni kwamba wengi wanaodai kuwa ni Wakristo na kudai kuwa Biblia ndiyo msingi halisi wa imani yao, wanashika zaidi mila za wanadamu, kuliko imani ya Biblia.

Katika masomo haya tutakuja kufikia kutambua kwamba Mungu kweli ni UPENDO (1 Yohana 4:8, 16) — siyo Mungu katili, wala mkali. Mungu anamtakia kila mmoja wetu awe na furaha, na AYAFURAHIE maisha kwa kiwango kamili, na kuyafanya maisha ya kusisimua. Sheria ya Mungu inaonyesha upendo (Marko 12:28-33; Yakobo 2:8) na ni njia iongozayo kutupeleka kwenye uzima (Torati 10:13; 30:19). Na pale TUTAKAPOANZA kuielewa Biblia, tutaikuta kumbe ni ya KUSISIMUA, ni yenye mvuto na pia ni yenye MANUFAA na ya kupendeza kuliko vyote.

Pale mtakapozama ndani ya Masomo haya, wengi wenu mtafurahia sana kujifunza huku kiasi kwamba hamtapenda kuchelewa kupokea somo linalofuata. Mtakuta kwamba vivutio na michezo ya kidunia SI BURUDANI, si YAKUFURAHISHA, si ya KURIDHISHA kiroho! Kwa sababu Mungu ni UPENDO, yeye ni mwumbaji wako akupendaye, na anahitaji wewe  uwe na furaha na afya  na mwenye mafanikio kupitia Biblia. Ni kupitia kwa NENO LAKE ndiyo hutumia kufunua kwako NJIA ya kutoka kwenye ukiwa, woga na mashaka, maradhi na magonjwa, umaskini na uhitaji, maisha matupu na yasiyo ya kuridhisha, na kukupeleka kwenye maisha ya furaha, afya,  na mafanikio TELE ambayo atakupa uyamiliki na kuyafurahia milele!

Tunapaswa kuelewa, kabla hata hatujaanza kujifunza Biblia yenyewe, kwamba SHARTI la kufikia uelewa sahihi ni KUJITOA kikamilifu katika utii kwa mafundisho yake, sheria zake na maelekezo. Yesu alisema tunatakiwa TUISHI kwayo (Mathayo 4:4) – sharti tujifunze ili kwamba kila tufanyalo tuhakikishe linaendana na maelekezo ya Biblia. Ndiyo kiongozi wetu katika maisha – iwe ni katika biashara, jamii na mahusiano ya kisiasa, yawe ni maisha ya kielimu ama ya kidini. Mungu anatufundisha TUJIFUNZE Biblia: “uonekane unakubalika kwa Mungu” (2 Timotheo 2:15). Yule ambaye hajifunzi kwa lengo hili – ambaye hajayatoa maisha yake kikamilifu kwa Mungu ili kwamba Mungu ayatawale maisha yake, huyo HAWEZI kuielewa Biblia, hata kama atajitahidi kiasi gani.

Ni kweli kabisa kwamba: “uelewa mzuri wanao wale wazishikao amri zake” (Zaburi 111:10) – na ni wale tu – ambao hawatamtii Mungu ndio ambao huwa hawapati uelewa sahihi! Na ni ndani ya Biblia ndiko ambako Amri zake zimetajwa na kufafanuliwa.

Tunaamini kwamba kozi hii ya Biblia itakuwa ya maana zaidi kwako endapo utauelewa uhusiano wake muhimu kwa  maisha yako na matukio ambayo yanatokea duniani. Uhusiano wake wa moja kwa moja na MATUKIO unayoyasoma kila siku kwenye magazeti, unayoyasikia radioni na kuyaona kwenye TV, ama hata kuyakuta kwenye internet. Ili kuelewa ni wapi mengi ya matukio haya yatatupeleka, ni lazima tuelewe, kwanza, kwamba INJILI YA YESU ilikuwa ni UJUMBE wa kimungu  uliotumwa TOKA KWA MUNGU KWA WANADAMU – ujumbe wa MPANGO WA MUNGU UNAOTEKELEZWA HAPA DUNIANI – uhusuo MWISHO WA ULIMWENGU HUU, na KUJA KWA UFALME WA MUNGU – ULIMWENGU WA KESHO utakaotimia hivi karibuni!

Endapo ungeifungua na kujaribu kuielewa ramani ya dunia, isingeeleweka vema kwako, hadi kwanza pale utakapopapata na kuweka kidole chako kwenye eneo sahihi la ramani hiyo paonyeshapo pale ulipo kwa wakati huo, na kisha ndipo ungeweza kuelewa vema maeneo mengine ya dunia, kulingana na yaliko kutokea kwenye eneo lako kwenye ramani hiyo, na ndipo kila eneo kwenye ramani litakapoeleweka. Sisi tunaamini utaweza kuielewa Biblia vema zaidi, na kuikuta ni ya kusisimua, ikiwa utaitafakari yote – historia yake na unabii wake – mafundisho na mafunuo yake matakatifu – kutokea kwenye kilele cha mtazamo utokanao na maisha yako. Ikiwemo, jinsi ulimwengu huu umejiendesha kufikia nyakati hizi zilizopo, na hali iliyopo, ambamo unaishi – ni wapi inaelekea kwenda baada ya hapa.  Utaikuta hii ni ya kusisimua zaidi na ni ya kuburudisha zaidi, na ni MUHIMU zaidi ya yote katika maisha yako endapo utajituma na KUJIFUNZA hasa!

KUMBUKA:  Hii Kozi ya Kujifunza Biblia ni Kozi ya KUJISOMEA BIBLIA. Siyo kitu ambacho unasoma tu harakaharaka. Kile tumekuandikia ni mwongozo tu wa kukusaidia UJIFUNZE BIBLIA. Kitu muhimu katika kozi hii ni kitabu cha BIBLIA! Daima hakikisha unayo Biblia yako pembeni yako kila uketipo kujisomea kozi hii. Ili ujifunze mengi toka kozi hii, jitahidi kukisoma kila kifungu cha maandiko kilichotajwa kuendana na kipengele unachosoma, siyo maandiko peke yake yale yaliyotajwa kujibu swali lililoulizwa katika mwisho wa kila somo. Yachunguze Maandiko ili ujihakikishie ikiwa yale unayofundishwa ni ya kweli (Matendo 17:11).

Unaishi katika Dunia ndani ya Machafuko!

Wengi leo wamejaa hofu, wakati wengine wamekata tamaa.

Hata wachambuzi wa maswala wengi leo wanalitambua hili kuwa kuna kitu kisichosawa kwenye ulimwengu huu. Wataletaje amani ya ulimwengu? Yapo mapendekezo kadhaa toka kwa wanadamu, lakini yote, yako kinyume na Mungu, na hivyo hayatafanikiwa (Warumi 3:17-18).

Wanasayansi wengi pamoja na wengine kwa ujumla wanasema wazi kwamba hadi tuwe na SERKALI YA ULIMWENGU mapema kuanzia sasa vinginevyo silaha kali za maangamizi zitaufuta uhai wote toka duniani. Lakini sasa  YAMESHINDWA KUFIKIA KWA AMANI, UUNDWAJI WA SERKALI YA ULIMWENGU! Umoja wa Mataifa, Mikutano ya Hague, Mkataba wa Paris, Kikao cha Berchtesgaden, Munich, Teheran, Yalta, pamoja na Potsdam vyote vilishindwa kuleta amani. Hata na Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa wala Marekani nayo imeshindwa (pamoja na jitihada za kuunda “Pax Americana”).

Kutokana na mabomu ya atomic na mabomu ya hydrogen, mabomu ya neutron, silaha za kemikali, silaha za kibayolojia, silaha za electro-magnetic pulse, pamoja na silaha zingine za teknolojia ya juu ambazo kwa sasa hazijulikani kwa walio wengi (ukichanganya na silaha zitakazozidi kuvumbuliwa na zinazoendelea kuundwa kwa sasa), wanadamu tunazidi kukaribia zaidi kwenye kipindi ambacho Yesu alituonya takribani miaka 2,000 iliyopita kuwa kingekuja, ambapo: “endapo Bwana hatazifupisha siku hizo, hataokolewa mtu akingali hai” (Marko 13:18).

Hakuna mwanadamu wala mnyama, samaki wala ndege ambaye angeepuka kuangamizwa na silaha hizi.

Ndiyo, ustaarabu wa ulimwengu huu umefikia kwenye JANGA! Je, uharibifu na uangamifu huo mbaya utokanao na hizo silaha utawafanya wanadamu wajizuie kuzitumia japo ziko mikononi mwa makundi ya vichaa wenye tamaa ya madaraka? Hilo halijawahi kuwazuia kutumia silaha hizo za maangamizi huko nyuma pale walipoona muda wa kufanya hivyo ulikuwa umewadia! Hata silaha za kemikali ambazo zimepigwa marufuku kidunia zinazoendelea kutengenezwa na wengine hata wanazitumia kuua wengi. MUDA WA KUTAFAKARI NA KUAMUA UMEWADIA! Wanadamu wanaonyesha wazi kuwa HAWANA KABISA uwezo wa kujitawala na kujiongoza wao wenyewe. Kwa kawaida, ukichaa wa kiongozi atakaye madaraka zaidi huishia pale tu yeye auawapo au kufariki—lakini sasa kila huyo aondokapo, viongozi wengine vichaa huibuka kuchukua sehemu yake kana kwamba walikuwa kwenye maandalizi na hivyo mbio za kuelekea kwenye uharibifu na uangamivu huzidi kusonga mbele!

Jibu ni nini?

MWANADAMU ATAANGAMIZANA MWENYEWE TOKA USO WA DUNIA, ENDAPO ATAACHIWA AENDELEE PASIPO MUNGU KUINGILIA KATI (Ufunuo 11:18)!

Wakati wengi wanatamani kuupuuza unabii na hawaamini juu ya zama hizi kufikia mwisho hivi karibuni, somo hili lilikuwa muhimu mno kwa Yesu kiasi kwamba alijibu maswali ya wanafunzi wake kuhusu hili:

“3 Hata alipokuwa ameketi kwenye Mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakisema, ‘Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa  zama?’

4 Yesu akajibu na kuwaambia: ‘Angalieni mtu asiwadanganye. 5 Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, ‘Mimi ni Kristo’, nao watadanganya wengi. 6 Nanyi mtasikia habari za vita na tetesi za vita. Angalieni msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia, lakini ule mwisho bado. 7 Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme. Kutakuwa na njaa, maradhi na matetemeko ya ardhi mahali mahali. 8 Haya yote ndiyo mwanzo wa utungu’” (Mathayo 24:3-8).

Yaonekana tuko katika nyakati ambazo Yesu alizitaja kuwa ndizo “mwanzo wa utungu” (Mathayo 24:8, Marko 13:8). Na kamwe hazitafuatiwa na nyakati njema kwa kuwa:  “Kwa kuwa wakati huo kutakuweko dhiki Kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe. Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingaliokoka mtu yeyote; lakini kwa ajili ya wateule siku hizo zitafupishwa” (Mathayo 24:21-22).

Iwapo hatuwezi kujiponya sisi wenyewe, NI NANI AWEZAYE KUTUOKOA?  JIBU la swali linatoka kwa yule ambaye ndiye neno lake limejaribiwa kwa zaidi ya mamia ya nyakati kupitia matukio yaliyokuwa yametabiriwa na Manabii wake, matukio ambayo yote yalitimia.

Huyu alikuwa ni nani? Yesu (Marko 13:20). Hatutakiwi kumwamini yeye pekee, bali tunatakiwa pia kuyaamini na yale aliyoyasema na kudumu ndani ya maelekezo yake (Yohana 8:31).

Kile alichokisema kuwa kinatakiwa kikuamushe wewe na mimi na kila mmoja wetu ni – “Wakati ni mfupi sana!” Ni dhahiri hautakuwa ukipoteza muda wako wakati utakapojifunza masomo ya kozi hii. Badala yake, utaJIFUNZA NJIA PEKEE ITAKAYOKUWEZESHA kujua MATUKIO MAKUU YAJAYO HIVI KARIBUNI. Utajipatia elimu ambayo itakuweka katika furaha kuu hapo baadaye. Jitihada zako katika hili zitakulipa maradufu kuliko chochote ambacho umewahi kutekeleza huko nyuma! Hivyo weka jitihada zako zote katika kujisomea masomo haya. Jinsi unavyoyasoma yaweza kuwa na matukio juu ya maisha yako ya baadaye na hususani juu ya sehemu yako katika maisha yajayo.

KWANINI Mungu Sharti Aingilie Maswala ya Ulimwengu

Wenye hekima WENGI, wasomi wa kiume na wa kike wanadhihaki wazo kwamba Yesu Kristo yu karibu kurejea. Hawaoni mantiki yoyote juu wazo hilo! Yawezekana hata wewe mwenyewe umewahi kuwafahamu watu wa aina hiyo, ama sivyo?

Katika karne ya 21, umbumbumbu wa Biblia na dhihaka waonekana kuongezeka sawa na Mtume Petro alivyotabiri kuwa hilo lingetokea wakati wa siku za mwisho (2 Petro 3:3-4).

Hawa ni matokeo halisi ya kizazi ambacho kimepoteza mtazamo wa ukweli wa kuwepo Mungu. Hudhihaki na kulipinga neno la Mungu ambalo hasa ndilo “neno la ukweli” (2 Wakorintho 6:7).

Jionee yafuatayo toka Kitabu cha Methali:

“7 Kumcha BWANA ndio mwanzo wa maarifa, Bali wajinga hudharau hekima na maelekezo” (Methali 1:7).

“29 Kwa kuwa walichukia maarifa wala hawakuchagua kumcha Bwana, 30 Hawakukubali maelekezo yangu wakayadharau maonyo yangu yote. 31 Kwa hiyo watakula matunda ya njia yao, na watashiba mashauri yao wenyewe. 32 Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza” (Methali 1:29-32).

“19 Maana hekima ya ulimwengu huu ni upuuzi mbele za Mungu.  Kwa maana imeandikwa, ‘Yeye ndiye awanasaye wenye hekima katika hila zao’; 20 na tena, ‘Bwana anayafahamu mawazo ya wenye hekima, ya kwamba ni ya ubatili’. 21 Basi, mtu yeyote asijivunie wanadamu” (1 Wakorintho 3:19-21).

Kizazi cha zama hizi kinajidai kuwa ndicho kilichoelimika zaidi, chenye majiji bora zaidi na chenye “werevu wa kidunia” kuliko wote waliowahi kuishi – lakini ndicho ambacho kimepoteza kabisa mwelekeo wa msingi wa elimu yote: Sisi ni nani, kwa nini tupo, KUSUDI la mwanadamu kuwepo ni nini! Iwapo hawa wasomi na wengine wote wangejua majibu kwa maswali haya, wangejua maana halisi ya SABABU na kwa kweli UMUHIMU HALISI – wa kurejea upesi – kwa Yesu Kristo kuja kuitawala dunia hii.

Lakini kwa vile ni wachache tu ndio wafahamuo, walio wengi wataangamia (Mathayo 24:24).

Machafuko ya Ulimwengu HAYAKWEPEKI!

Pamoja na jitihada za dhati kujaribu kuleta amani inayodumu – VITA KAMILI inazidi kutusogelea. Kuibuka kwa bomu la hydrogen – uwezekano wa KUANGAMIZWA DUNIA NZIMA sasa ni kitu halisi! Japo tumeonywa kwamba jibu pekee ni kuwepo kwa SERKALI YA ULIMWENGU—jitahada za kibinadamu za kufikia azima hii ZOTE ZIMESHINDWA VIBAYA.

Wanasiasa na wanasayansi mbalimbali wameanza kutambua hili linamaanisha nini. Baadhi wanaanza kuogopa! Ukweli wazi na wa kutisha ni kwamba WANADAMU TAYARI WAMESHAFIKA MWISHO WA KAMBA YAO. Wanadamu wamefikia pale ambapo hawawezi tena kujilinda wao wenyewe dhidi ya silaha za kuogofya walizojitengenezea wao wenyewe. KUINGILIA KATI KWA MAMLAKA YA JUU NDIYO NJIA PEKEE TULIYONAYO KWA MAOVU YA ULIMWENGU HUU.

Wakati Yesu alipokuwa hapa duniani, alifahamu ni wapi ubunifu wa wanadamu ungewafikisha wakati wa miaka ijayo. Yesu alijua kuwa katika wakati huu wa mwisho watu wangekuwa wakipapasa gizani kuitafuta njia ya kufikia amani, lakini kwa kweli wangeishia kwenye ukingo wa kuuangamiza uhai wote: “Kama siku hizo zisingalifupishwa, asingaliokoka (asingalibaki hai) mtu yeyote,” Kristo alionya (Mathayo 24:22).

Chanzo cha Majanga ya Ulimwengu

Katika unabii huu wa kustaajabisha, Yesu pia anatupa ufunguo juu ya KWANINI ulimwengu wetu wa sasa uko katika hali mbaya. Alionya: “Lakini kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa wakati wa kuja kwake Mwana wa Adamu” (Mathayo 24:37).

Ni kipi walichokuwa wakifanya wanadamu enzi za Nuhu maelfu ya miaka iliyopita, ambacho kiliwasababishia waishie kwenye uangamifu mkubwa?

Ifungue Biblia yako kwenye Mwanzo 6:12-13 ambako ndiko tunalikuta jibu: “Mungu akaiangalia dunia, na tazama imepotoka; maana kila mwenye mwili amejiharibia njia yake duniani. Mungu akasema… wameijaza dunia dhuluma.”

Wanadamu wa asili wametumia fikra zao za kibinadamu na kuondoka toka njia ya maisha ambayo Mungu aliwapa hapo mwanzo. Mabadiriko haya ya kuiacha NJIA ya Mungu na kugeukia KIKRA ZA KIBINADAMU POTOFU ndicho kinachotishia kuangamia kwa ulimwengu. Yesu alisema hali hiyohiyo ndiyo itakayokuwa imeshamiri punde tu kabla ya kuja kwake mara ya pili.

Ebu uangalie ulimwengu huu unaokuzunguka.

Jionee kile ambacho Mtume Paulo alivuviwa kuandika:

“18Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni dhidi ya uasi wote na uovu wa wanadamu ambao huipinga kweli kwa uovu wao, 19kwa maana yote yanayoweza kujulikana kumhusu Mungu ni dhahiri kwao, kwa sababu Mungu mwenyewe ameliweka wazi kwao. 20Kwa maana tangu kuumbwa kwa ulimwengu, asili ya Mungu asiyeonekana kwa macho, yaani, uwezo Wake wa milele na asili Yake ya Uungu, umeonekana waziwazi ukitambuliwa kutokana na yale aliyoyafanya ili wanadamu wasiwe na udhuru.

21Kwa maana ingawa walimjua Mungu, hawakumtukuza Yeye kama ndiye Mungu wala hawakumshukuru, bali fikira zao zimekuwa batili na mioyo yao ya ujinga ikatiwa giza. 22Ingawa wakijidai kuwa wenye hekima, wakawa wajinga 23na kubadili utukufu wa Mungu aishiye milele kwa sanamu zilizofanywa zifanane na mwanadamu ambaye hufa, ndege, wanyama na viumbe vitambaavyo.

24Kwa hiyo, Mungu akawaacha wazifuate tamaa mbaya za mioyo yao katika uasherati, hata wakavunjiana heshima miili yao wao kwa wao. 25Kwa sababu waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakaabudu na kutumikia kiumbe badala ya Mwumba, ahimidiwaye milele! Amen.

26Kwa sababu hii, Mungu aliwaacha wavunjiane heshima kwa kufuata tamaa zao za aibu. Hata wanawake wao wakabadili matumizi ya asili ya miili yao wakaitumia isivyokusudiwa. 27Vivyo hivyo wanaume pia wakiacha matumizi ya asili ya wanawake wakawakiana tamaa wao kwa wao. Wanaume wakafanyiana matendo ya aibu na wanaume wengine nao wakapata katika maisha yao adhabu iliyowastahili kwa ajili ya upotovu wao.

28Nao kwa kuwa walikataa kumkubali Mungu, Yeye akawaacha wafuate akili zao za upotovu, watende mambo yale yasiyostahili kutendwa. 29 Wakiwa wamejawa na udhalimu wa kila namna, uasherati, uovu, tamaa mbaya na hila. Wamejawa na husuda, uuaji, ugomvi, udanganyifu, hadaa na nia mbaya. Wao pia ni wasengenyaji, 30wasingiziaji, wanaomchukia Mungu, wajeuri, wenye kiburi na majivuno, wenye hila, wasiotii wazazi wao, 31wajinga, wasioamini, wasio na huruma na wakatili. 32Ingawa wanafahamu sheria ya haki ya Mungu kwamba watu wanaofanya mambo kama hayo wanastahili mauti, si kwamba wanaendelea kutenda hayo tu, bali pia wanakubaliana na wale wanaoyatenda” (Warumi 1:18-32).

Gundua kwamba tabia zilizopo leo miongoni mwa wengi zitatupeleka kwenye kuangamia. Si tu kwa wale wanaozitenda, bali hata na kwa wale wanaozikubali na kuziruhusu!

Je wanadamu wamekuwa wakimtafuta Mungu na kuifuata njia yake – ama siku zote wanafuata fikra za kibinadamu kuhalalisha kuendelea katika njia yao wenyewe? Sawa na Mtume Paulo alivyoandika juu ya wote waufuatao mwili:

“16 maangamizi na taabu viko katika njia zao, 17wala njia ya amani hawaijui.18 Hakuna hofu ya Mungu machoni pao” (Warumi 3:16-18).

 

Jisomee utafakari sura hii yote kwa makini.

Pointi muhimu katika kuuelewa mpango wa Mungu imeonyeshwa hapa.

Elewa kwamba Mungu anazungumzia juu ya NJIA maalum ya kuiendea amani – na kwamba anaunganisha kutoijua na kitu kimoja: kutokuwa na aina sahihi ya utii na uoga (kumcha) – WOGA wa kimungu. Msingi wa tabia ya utii na heshima hata kufikia KUYABEZA MATAKWA NA MAMLAKA YA MUNGU na ndiyo hali halisi iliyopo miongoni mwa watu wa kila aina ya jamii katika maisha ya leo. Katika “kizazi chetu kilichostarabika” kama tujiitavyo, wanadamu hawaogopi kutenda uovu.

Hili limetupeleka wapi?

Katika Marekani, kutaja mfano mmoja, kuongopa kunachukuliwa kuwa ni haki inayolindwa na katiba ya nchi hiyo kulingana na maelezo ya Mahakama Kuu yao. Kila kitu kimewekewa ufunguo wa neno la siri kukifikia (passwords) na kupata habari zake. Kila mahali kumetapakaa uvunja sheria na umwagaji damu (Ezekieli 7:23).

Watu sasa wanaanza kutambua kwamba kuna tatizo ndani ya jamii hii ya ulimwengu. Na lililodhahiri hata zaidi ya JANGA LINALOZIDI KUONGEZEKA la uvunjaji sheria ni kule kutambua kuwa katika kizazi chetu DUNIA YOTE IKO HATARINI kutokana na majasusi, wauaji wa kujitoa muhanga, madikiteta  wa mataifa makubwa ambao sasa tayari wamejipatia uwezo wa kuufuta uhai wote toka sayari hii. Na siyo toka mataifa ama kundi la mataifa pekee ambayo yanaonekana kupenda vita kwamba wao ndio tishio pekee (Isaya 10:5-11).

Imetabiriwa!

Nyakati hizi za kutisha zimetabiriwa na kufafanuliwa katika Biblia yako. Fungua Biblia yako sasa kwenye 2 Timotheo 3:

1 Lakini yakupasa ufahamu jambo hili, kwamba siku za mwisho kutakuwa na nyakati za hatari. 2Kwa maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kumkufuru Mungu, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio watakatifu, 3wasio na upendo, wasiopenda kupatanishwa, wasingiziaji, wasiozuia tamaa zao, wakatili, wasiopenda mema, 4wasaliti, wakaidi, waliojaa majivuno, wapendao anasa zaidi kuliko kumpenda Mungu. 5Wakiwa na mfano wa utauwa kwa nje lakini wakizikana nguvu za Mungu. Jiepushe na watu wa namna hiyo” (2 Timotheo 3:1-5).

Paulo alivuviwa kumwandikia Timotheo juu ya siku za mwisho—karne hii ya 21, pale USTAARABU wenyewe utakuwa hatarini kutoweka!

Fuatilia kwa makini hali ya kumomonyoka maadili ya wanadamu wa siku zetu. Ndiyo, mataifa yote siku hizi yanatamani mali za wengine na yako tayari KUUA NA KUANGAMIZA ili wazipate. Badala ya kumtafuta Mungu Mwenyezi, mataifa yaliyo mengi hujivunia uwezo wao wa majeshi na silaha zao za maangamizi. WANAMKUFURU Mungu bila kukoma kwa maneno na vitendo.

Mbele za Mungu, wengi leo ni wakorofi. Wengi wana “muonekano wa uchamungu,” lakini wanakana nguvu zake za kujiingiza kwenye maswala ya ulimwengu na mamlaka yake ya KUTAWALA maisha yao binafsi ama wote pamoja. Watu katika kila taifa yaonekana wame pania kutenda mambo kivyao kinyume na Mungu wa kweli wa Biblia.

Njia hiyo inapeleka kwenye MAUTI. Mungu alimuvuvia Yeremia kuandika kwamba: “Moyo ni mdanganyifu kupita vyote, unaugonjwa wa kufisha” (Yeremia 17:9). Asili ya mwanadamu haijabadirika! Lakini wasomi wengi na watu wengine wanajidai kutenda kana kwamba imebadirika.

Kumbuka Kristo alisema hali katika ulimwengu huu kabla ya kuja kwake ingekuwa: “kama katika siku za Nuhu” (Mathayo 24:37). Tofauti na siku za Nuhu, mwanadamu kwa sasa anao uwezo wa kufutilia mbali uhai wote haraka na mara moja utoke katika sayari hii – tena kwa njia nyingi tu.

Mwanasayansi wa Kiingereza Sir Robert Watson – Watts, mvumbuzi wa kwanza wa mawasiliano ya “radar”, anasema, anafunua yafuatayo kwamba: “Sina matumaini kuwa mwanadamu ataendelea kuishi kwa maika 10 mingine ijayo”. Anataja kuwa kuna NJIA TATU ambazo wanadamu wa ULIMWENGU WANAWEZA KUFUTILIWA MBALI ndani ya masaaa MACHACHE tu . Ya kwanza ni BOMU la Hydrogen, Ya pili ni silaha kali ya sumu ya “Toxin” iwezayo kutengenezwa kutoka kimelea kiitwacho BOTULINUS. ‘‘Inahitajika KIASI CHA KILO MOJA TU kuweza KUUA wanyama na WANADAMU WOTE WA ULIMWENGU”, anaonya kwa hofu! “Tena inatengenezeka kwa urahisi tu, inajulikana kiasi kikubwa, na, kundi lililofundishwa vema, laweza kuitumia sumu hii kuangamiza. Kama aina ya tatu ya silaha ya maangamizi ya wanadamu, alizitaja silaha za GESI za NEVA (NERVE GASES). Njia tatu za maangamizi ya Ulimwengu wote!

Tafakari hayo!

Miongo kadhaa, Sir Robert Watson na Dr. Brock Chisholm, wa Victoria “waliunganisha nguvu kuuelimisha ulimwengu juu ya elimu ambayo sasa haikutakiwa ibaki siri” (Daily Sun, Vancouver, B. C., Jan. 21, 1959). Afisa mmoja wa juu toka ofisi za jeshi la Marekani – Pentagon, huko Washington, D. C., aliliweka wazi jambo hilo: “Tuko katika hofu kuu kiasi cha kufa hata kutaja tu juu ya silaha za kimelea (Botulinus)”.

Na tokea wakati huo hadi sasa kiwango cha uangamizaji kimezidi kuongezeka.

KITU FULANI CHA MUHIMU LAZIMA KIFANYIKE la sivyo mwanadamu atajiangamiza kabisa yeye mwenyewe.

Tumaini Moja Tu

Msingi wa chanzo cha machafuko ya ulimwengu, na kimsingi – ufumbuzi wake, imefafanuliwa kwa ufasaha na wanasiasa wawili marehemu wa Kimarekani. Katika hotuba yake ya kutawazwa, Rais Dwight D. EISENHIOWER Alieleza:

“Katika matukio makuu yapitayo kasi, tunajikuta tukipapasa kutafuta kujua maana halisi na kusudi la nyakati ambazo tunaishi… Ni mbali kiasi gani tumesafiri katika safari ndefu ya mwanadamu kutoka gizani kuelekea kwenye nuru? Je, tunaikaribia nuru—siku ya uhuru na amani kwa wanadamu wote? Ama ni vivuli vya usiku mwingine vinatunyemelea kwa kasi? . . . Sayansi yaonekana iko tayari kututunuku juu yetu, kama zawadi yake ya mwisho, UWEZO WA KUUFUTA UHAI WA MWANADAMU TOKA SAYARI HII”.

Ndiyo,  anaelewa—anatambua kwamba mwanadamu anaweza kujiangamiza mwenyewe. Kisha baada ya kuainisha kanuni tisa ambazo zingeongoza mahusiano ya kimataifa, alitamka ukweli ambao—Iwapo ungetumika kwa usahihi – ungekuwa hatua kubwa kuelekea kwenye suluhisho, si wa matatizo yetu pekee, bali na wa ulimwengu wote. Alisema: “Kwani ukweli huu sharti ueleweke kwetu sote: Chochote ambacho America inataraji kukileta kipokelewe ulimwenguni sharti kwanza kipokelewe ndani ya MIOYO ya Wamarekani”.

Iwe alilitambua hili ama la, Rais Eisenhower aliongea sawa kabisa na maneno ya Mungu wakati wa hotuba yake hiyo kwamba katika America—sawa na katika mataifa mengine—moyo, TABIA za wanadamu sharti zibadirike ikiwa tunahitaji kupata amani duniani.

Ebu sasa na tufuatilie maneno ya kipekee na mazito yaliyotamkwa na mtu mashuhuri, marehemu Generali Douglas MacArthur kuhusu swala hili. Pale alipopumzishwa jukumu la kuongoza kikosi cha jeshi na kuagizwa arejee Marekani na Rais Truman, GENERALI MACARTHUR alitoa HOTUBA ya kihistoria mbele ya kusanyiko la Bunge la Marekani. Katika hotuba hiyo ya kusisimua, alitoa maelezo makuu yaliyobainisha weredi wake, alisema:

“Ninaijua vita sawa na watu wengine wachache sana waishio sasa wanavyoijua, na hakuna kingine kwangu mimi—na hakuna kingine kwangu kinachochukiza zaidi…., Wanadamu tangu mwanzo wa nyakati wameitafuta amani. . . Ushirikiano wa Kijeshi, jitihada za kulinganisha nguvu, Umoja wa Mataifa, yote haya moja baada ya jingine yameshindwa, yakiacha njia pekee kuwa ni kwa kupambana katika vita. Uangamifu mkubwa wa vita sasa unaiziba njia hii kuwa haifai tena. TUMEVUKA FURSA YETU YA MWISHO SASA. Iwapo hatutabuni mfumo mbadala na ulio bora zaid kwa sasa, “HAL—MAGEDONI” yetu itatunyemelea mlangoni. Tatizo letu kimsingi ni la KITHEOLOJIA na LINAHUSU kuwa na roho iliyopondeka zaidi na KUBADIRIKA KWA TABIA YA MWANADAMU ili iendane na mwelekeo wetu wa kasi ya maendeleo  ya kisayansi, sanaa, fasihi pamoja na dhana na maendeleo ya kiutamaduni ya miaka 2000 iliyopita”. “NI SHARTI ITOKANE NA ROHO IWAPO TUNATAKA KUUOKOA MWILI”.

Ebu na tuyatafakari maneno haya ya nguvu. Pamoja na kwamba huyu alikuwa ni Jemedari mashuhuri, MacArthur aliamini kwamba—katika vita ya dunia—tulikuwa tayari tumepitia fursa yetu ya mwisho! Wanajeshi wote hawa walijua wazi kabisa kwamba SULUHU PEKEE – TUMAINI pekee la kuepuka kuangamia kwa wanadamu—ilikuwa ni kubadirika kwa roho ya mwanadamu – kubadirika kwa mwenendo wa watu uelekeao kupenda uovu (Mhubiri 7:9; Ezekieli 11:19-20) —kuijenga upya TABIA ya mwanadamu.

Jibu

Iwapo wanadamu waliopotoka wangeachiwa wenyewe kwa muda wa kutosha walete ufumbuzi wa matatizo ya ulimwengu huu, hatima yake ingekuwa KUANGAMIA kwa dunia (Mathayo 24:22; Marko 13:19-20).

Watu wengi wanakusudia kufanya mambo sahihi, lakini hawaijui njia ya kuelekea kwenye amani. Wanadhamira ya kweli, lakini kweli wamepotoka. Sawa na Selemani alivyovuviwa kutuandikia: “Iko njia ionekanayo kuwa ni sahihi mbele ya mwanadamu, lakini hatima yake ni njia za MAUTI” (Methali 14:12).

Mungu anabainisha kwamba njia ya kawaida, ambayo mtu wa tabia ya asili anaitamani kuifuata huishia kwenye mauti. Watu daima hudanganyika kwa kudhani kwamba hakuna hatari yoyote kwa sasa – kwamba siku zote ulimwengu umekuwa hivihivi. Hii ni kweli kwa sehemu fulani.

Asili ya mwanadamu daima imekuwa hivi siku zote. Mtu wa tabia za kimwili siku zote kaleta mauti na uangamifu kwa ulimwengu. Hata hivyo, kumbuka kwamba Paulo alisema: “Bali watu waovu na wazinzi watazidi kuwa waovu zaidi na zaidi” (2 Timotheo 3:13). Na la muhimu kupita yote, KUANGAMIZWA KWA WANADAMU WOTE HAKUJAWAHI KUWEZEKANA KABLA YA NYAKATI ZA VITA YA II YA DUNIA – na sasa imezidi kuwa hatari zaidi.

Mwanadamu katengeneza bunduki na mizinga siku nyingi zilizopita. Baadaye, vifaru na ndege za kivita zikaanza kutumiwa. Lakini kwa sasa tunazo roketi ziwezazo kubeba silaha za “hydrogen missiles” na kuweza kuangamiza miji kadhaa kwa kubonyeza swichi ya “remote” tu! Inaaminika kwamba mabomu ya “electromagnetic pulse”, ikiwa yatalipuliwa sehemu iliyokusudiwa, yanauwezo wa kuurudisha ulimwengu wa nchi kama za magharibi hadi karne za enzi za mawe. Uwezekano wa kuangamia kwa wanadamu siyo jambo la kukisia tu bali ni ukweli wa kuogofya!

Na sasa hakuna kiwezacho kumwokoa mwanadamu toka kujiangamiza mwenyewe bali tu ni KUBADIRIKA kwa asili ya mtu – katika tabia ya wanadamu. Lakini pamoja na utele wa makanisa yajiitayo kuwa ya “Kikristo” – pamoja na jitihada finyu za Umoja wa Mataifa – pamoja na jitihada zote anazozifanya mwanadamu kuleta amani na furaha, VITA KAMILI inazidi kutusogelea. Japo kutakuwepo nyakati zionekanazo kuwa ni za amani, matangazo ya amani na usalama yatatolewa punde tu kabla uangamifu utujiapo kwa ghafla (1 Wathesalonike 5:3). Cha kusikitisha, wengi watawaamini wale watakaotangaza kuja kwa amani ya uongo isiyo chini ya Mungu wa Biblia (Ezekieli 13:10-16).

Sawa na Suleimani alivyovuviwa kuandika: “NJIA IONEKANAYO KUWA NJEMA MACHONI MWA WANADAMU DAIMA NI NJIA YA MAUTI”. JIBU NI LIPI? NI MUNGU PEKEE NDIYE AWEZAYE KUIBADIRI TABIA YA MTU, na kuwalazimisha wanadamu kujifunza njia ya amani.

Hiyo ndiyo SABABU inayomrudisha Kristo kuja kuchukua “Falme za Ulimwengu huu” (Ufunuo 11:15).

Hiyo ndiyo SABABU “Yeye mwenyewe ndiye atawatawala kwa fimbo ya chuma” (Ufunuo. 19:15). Hiyo ndiyo njia pekee ya kuyaokoa maisha ya mwanadamu yasitoweke toka sayari hii. Yesu Kristo alijua juu ya hali mbovu ya maswala ya watu ambayo wangejiletea wenyewe katika siku hizi za mwisho, pale aliposema: “Na kama siku hizo zisingalifupizwa, HAKUNA MWANADAMU ANGEOKOLEWA HAI” (Mathayo 24:22).

Mungu na akusaidie uelewe umuhimu na uhalisi wa mambo haya kadri usomapo makala hizi.

Zinaonyesha kwamba Mungu aliona kabla juu ya kubuniwa na kuundwa kwa silaha tulizonazo leo za maangamizi makuu mapema kabla hata mwanadamu hajawahi kuota kuwa angeziunda. Na zinafunua kuwa Mungu tayari alikuwa amebuni suluhisho pekee na la maana. Mpango wote kamili wa Mungu ni wa maana na halisi.

Muundo wa MPANGO wa Mungu usioeleweka sana kwa wengi umetolewa ndani ya sura za kwanza mbili za kitabu cha Mwanzo. Ni JUMA la siku saba.

Sawa na Mungu alivyozianzisha nyakati pale mwanzo, mwanadamu amepewa siku sita za kazi zinazofuatiwa na siku ya mapumziko. Katika Waebrania 4:4, 11, siku ya saba pia ni kivuli cha pumziko la amani—pumziko la miaka 1,000 ambalo litafuatia kizazi chetu hiki cha kazi za wanadamu za mahangaiko na taabu duniani.

Fuatilia kwa umakini pumziko lenye amani la baada ya Kristo kujiingiza na kuanzisha utawala wake liitwalo “akatawala miaka elfu” (Ufunuo 20:4). Iwapo “siku ya mwisho” ya mpango wa Mungu wa miaka 7,000 – ni miaka 1,000, basi zile SIKU SITA ALIZOZITENGA KUTUMIWA NA WANADAMU kwa KAZI nazo ni dhahiri zitakuwa sawa na miaka 6,000.

Na hili ndilo hasa matukio ya ulimwengu yanalolithibitisha.

Tazama hali ilivyo! Ulimwengu huu unaelekea kuangukia kwenye KUANGAMIA!

Ukijumulisha miaka mbalimbali ya watu wa Kitabu cha Mwanzo, miaka ya utawala wa wafalme mbalimbali, na kuongezea tarehe za matukio kadhaa ya kwenye Biblia, utakuta kwamba miaka 6,000 ya wanadamu kujisimamia ni dhahiri imefikia kikomo.

Kwa maneno mengine MFUATANO WA MATUKIO YA ULIMWENGU unathibitisha tuko KARIBU SANA na muda ambao maandiko siku zote yameusema kuwa KRISTO ATAREJEA – pale udhahiri wa kufikia kwa muda wa dunia kujiangamiza utafika. Miaka elfu sita ya historia ya mwanadamu umfikia ukingoni. Hapa, sasa, tunakupa uthibitisho-UTHIBITISHO MARA DUFU—kuwa KRISTO ANAKUJA katika nyakati za kizazi chetu!

Mtazamo kuwa wanadamu wameishi katika dunia kwa makumi ya maelfu ya miaka iliyopita ni ngano isiyoweza kuthibitishwa! SAYANSI yenyewe inaithibitisha kuwa si kweli! Hata kama itaonekana kuwa hili ni la ajabu, nadharia ya kuwa mtu katokana na mabadiliko “evolution” nayo si kwamba tu haithibitiki, bali pia inathibitika kuwa ni upuuzi pale tunapoelewa ukweli.

Somo lifuatalo punde litakupa kweli hizi ili uweze kujifunza mwenyewe nyumbani! Hata Mitume nao hawakuwa tayari wamepata uelewa juu ya MPANGO WA MUNGU huu pale Kristo alipokuwa angali hapa duniani. Walifikiri ufalme ungesimikwa wakati wa nyakati zao, ilipokuwa bado ni miaka 4,000 tu ya mpango wa Mungu ndiyo pekee iliyokuwa imekamilika.

Lakini kabla hawajafariki, MITUME WALIKUWA TAYARI WAMEUJUA MPANGO WA MUNGU. Petro alisema: “Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake (ya kuja kwa Kristo) . . . bali anavumilia” (2 Petro 3:9).

Mungu yu mvumilivu.

Mungu amejizuia kuingilia katika maswala ya ulimwengu kwa takribani miaka 6,000.

Kwa nini?

Sababu hawezi kuingilia hadi pale mwanadamu atakapofikia kumlilia Mungu baada ya kukabiliwa na janga la kujiangamiza mwenyewe. Elewa kwamba siku ya Kristo kujiingiza na kutawala imelinganishwa na “miaka elfu moja” (Ufunuo 20:4; Zaburi 90:4).

Petro pia anasema kitu kilekile—kwamba siku moja machoni kwa Mungu ni sawa na “miaka elfu moja” na “miaka elfu moja ” ya maisha ya ustaarabu wa mwanadamu ni sawa na siku moja katika mpango wake wa juma moja la miaka elfu moja moja—ya siku saba (2 Petro 3:8).

KRISTO ANAREJEA BAADA YA SIKU SITA ZA MIAKA ELFU MOJAMOJA ya mahangaiko na taabu ya utumwa wa mwanadamu. Wafuasi wa kweli wa Kristo kwa miaka mingi wametambua kwamba Mungu atamtuma Yesu Kristo kuja kuusimika ufalme wake katika mwaka wa siku ya saba ya miaka elfu moja, ambao utaleta nyakati za mapumziko na amani.

Ni wa KUSISIMUA kiasi gani kwamba ni katika nyakati zetu hizi pale ambapo miaka 6,000 tayari IMEFIKIA KIKOMO, ndipo ulimwengu umetiishwa na kuangamizana. Ni wa KUTIA MOYO kiasi gani kwamba Yesu mwenyewe alisema kwamba pale tutakapoyaona haya yote yakitokea tujue YU KARIBU KURUDI!

Biblia ni Nini?

Neno Biblia linatokana na neno la Kigiriki biblio linalomaanisha kitabu.

Pale kozi hii (sawa na wengine wengi) litumiapo neno “Biblia” au “Biblia Taklatifu” hii inataja vitabu 39 vinavyoaminika kuwa ni “Maandiko” yaliyo andikwa hapo awali kwa Kiebrania na Wayahudi (yajulikanayo kuwa ni maandiko ya Kiebrania ama Agano la Kale), pamoja na vitabu 27 vinavyoaminika kuwa ni maandiko na hapo awali viliandikwa kwa Kigiriki na wale waliokuwa wanafunzi wa Yesu Kristo (yajulikanayo kama maandiko ya Kigiriki ama Agano Jipya). Maandishi yaliyomo katika Biblia yanachukuliwa kuwa ni “Maandiko”.

Hakuna kitabu chochote cha Biblia kilichoandikwa hapo mwanzo kwa lugha ya Kilatini na wala hakuna kilichokuwa hapo mwanzo kimeandikwa kwa Kiingereza ama Kiswahili. Hivyo Biblia ya zamani ya Kilatini cha kale “Vulgate” iliyoandikwa na Jerome ambayo wengi wa Wakatholiki waliitumia pamoja na Biblia mashuhuri iitwayo “King James Version” ambayo wengi wa madhehebu ya Kiprostanti hupenda kuitumia vyote ni tafsiri ambazo MUNGU HAKUZIVUVIA MOJA KWA MOJA sawa na Maandiko ya awali! Hizi ni tafsiri zilizotokana na tafsiri tena zingine kiasi cha kupoteza baadhi ya maana zilizokusudiwa hapo awali. Mara nyingi tafsiri huwa na makosa ambayo aidha yalikusudiwa ama yalikuwa ya bahati mbaya.

Maandiko ya awali kabisa ya Biblia hayapo tena kwani yalioza, ama kupotea au hata yaliharibiwa. Hata hivyo, bado kuna maandiko mengi ya awali ambayo yanapatana na Biblia zilizotafsiriwa kwa usahihi, yanayoithibitisha kuliko maandiko mengine ya maelfu ya miaka ya kale. Wayahudi, kwa mfano, walikuwa na utaratibu makini sana wa kunakiri na kuhakiki ili kudhibiti upotezaji wa maana ya awali ya maandiko. Agano Jipya lenyewe lilikuwa na nakala nyingi zilizosambaa kwa wengi ndani ya kipindi kifupi baada ya kuandikwa kwake ili kuhakikisha kutotokea kupotea ama kubadirishwa kwa maana ya awali ya Maandiko.

Lakini sasa ni toleo lipi la maandiko ya awali ndilo liwe msingi wa kutumika wakati wa kutafsiri imekuwa ni hoja yenye mkanganyo. Toleo la “Nestle-Aland NA27” la kigiriki la Agano Jipya (NA27/UBS4) lenyewe hudai kwamba lilitumia matoleo yote ya Kigiriki ya Agano Jipya yaliyokuwepo wakati wa utafasiriwa wake, na kwa kawaida linadai ndilo lililo karibu zaidi na maandiko ya awali (na wala halikuweka maandiko batiri kama yale ya 1 Yohana 5:7-8 ambayo tafsiri ya “Textus Receptus” inayo). Japo hii haimaanishi kwamba toleo la NA27 halina makosa; ni maandiko ya awali ndiyo yanafaa, na inaonekana maandiko yaliyotafsiriwa toka toleo hili ndiyo yakubalikayo na wengi kuwa yako sawa na yale ya awali “Traditional Text”—ambako ndiko matoleo ya “Textus Receptus” yalitoka—ambayo ndiyo yalikuwa maandiko yatumiwayo na kanisa la kale la Asia Ndogo na lile la Byzantium.

Cha ajabu, pale makanisa ya Kigiriki na Kirumi yalipoanza kupinda kutoka kwenye mtazamo wa Kibiblia juu ya Uungu wakati wa mwishoni mwa karne ya nne, makanisa haya yalianza kupunguza kutegemea “Maandiko ya Awali” kama mwongozo na wakati mwingine yakatumia zaidi nyaraka ambazo hazikuwa sahihi na hazifai kutumiwa (Burgon JW. The Causes of the Corruption of the Traditional Text of the Holy Gospels. Cosimo Classics, 2007, p. 2).

Nje ya ulimwengu wa Kirumi na kiorthodox ya masahariki, tafsiri mbili miongoni mwa zile zilizokuwa zikitumika sana zilizo za kiingereza ni ile tafsiri ya “King James Version” (KJV) ya mwaka 1611 na ile ya “New Kings James Version” (NKJV) ya mwaka 1982. Hizi zote zilitafsiriwa ili zilete maana ya neno- kwa – neno ambapo (KJV imetokana na toleo la “Textus Receptus” na  NKJV ikiwa imechanganya, toleo hili na pia baadhi ya “Maandiko ya Awali” na mengine ambayo waliotafsiri KJV hawakuweza kuyapata). Tafsiri za neno-kwa-neno ni bora zaidi kwa kujifunza Biblia kuliko zile zilizofafsiriwa kwa kufuata maana ya aya katika Biblia. Tafsiri ya kuonyesha maana ni jitihada za yule anayetafsiri kutoa maana ya aya ama sura ile anayoitafsiri kwa kufuata kile anachoona, anachodhani, ama anachokiamini kuwa maandiko ya awali yalimaanisha, kinyume na kutafsiri ya kila neno jinsi lilivyo na hivyo kumwacha msomaji aamua mwenyewe lengo la aya ama sura. Lakini kwa kuwa tafasiri hizi za maana ni nyingi na rahisi kuzisoma kuliko zile za neno-kwa-neno, wengi huzipendelea.

Kwa usomaji wa kila siku mimi siku hizi hupendelea kutumia tafsiri ya Biblia ya “New Kings James Version” (NKJV) kwa kuwa ndiyo iliyo miongoni mwa zilizo sahihi zaidi; ndiyo inayo makosa ya utafasiriji lakini pia inatumia lugha ya siku hizi. Nimesoma tafasiri nyingi mbalimbali kwa ukamilifu.

Huko nyuma nilizoea kutumia tafsiri ya KJV zaidi, lakini ni ngumu kwa walio wengi kuielewa – kwa kuwa wengi wa watu wa siku hizi wanashida ya kukielewa Kiingereza cha kale na wengi wa walio si wazaliwa wa lugha hiyo hupata shida sana. Pamoja na KJV, ijapokuwa wengi huiamini sana, lakini tafsiri hiyo inayo makosa mengi (imeitafsiri vibaya aya ya Matendo 12:4, Waebreania 4:9, 1 Yohana 5:7-8, na kadharika) – kiukweli tafsiri hii si bora kuliko tafsiri nyingine zote zilizopo kama wengi waaminivyo!

Ni muhimu ieleweke kwamba Biblia haikuwahi kueleza kwamba Roho ya Mungu ingewaongoza wale watakaotafsiri Biblia toka lugha za awali kwenda lugha za mataifa mbalimbali (kama ambavyo wengi watumiao KJV na wale wa Septuagint wanavyodai na Kuamini).

Nyakati zingine kwa ajili ya ufafanuzi, nitanukuru toka NIV (New International Version). Japo tafsiri hii siyo mahala pote ya neno-kwa-neno, nyakati nyingine imeyaweka baadhi ya maneno kwa usahihi zaidi kuliko NKJV au KJV.

Katika makala ziongeleazo maswala ya Kikatholiki nitaweza kutumia tafsiri ya  Douay Rheims (DRB) ya mwaka  1610 ama tafsiri iliyoifuatia—lakini kwa kuwa ni tafsiri toka tafsiri nyingine (Jerome aliitafsiri Biblia kwenda Kilatini karibia na mwisho wa karne ya nne na Douay-Rheims ni tafsiri ya Kiingereza iliyotokana na ile ya Kilatini ya Jerome). Sipendekezi kwamba itumike kama tafsiri tegemeo. Wakatholiki pia hutumia tafsiri ya “New Jerusalem Bible” (NJB)—ambayo ni tafsiri ya neno-kwa-neno zaidi kuliko ile ya DRB, japo wakati mwingine inayo makosa yake. NJB yaonekana kuwa ndiyo tafsiri ya Biblia ya Kiingereza itumiwayo zaidi na Wakatholiki nje ya Marekani. Na kwa vile inatumia zaidi lugha ya siku hizi, naiona NJB kuwa ya msaada zaidi, hususani pale nilengapo jamii ya watu wa asili ya Kikatholiki zaidi.

Wakati mwingine inasaidia ukisoma tafsiri kadhaa juu ya aya ama sura fulani unayojifunza kwani yaweza kukusaidia kuelewa zaidi, japo wakati mwingine makosa ya tafsiri yaweza kuwa tatizo. Lakini kadri ujisomeapo Biblia mara kwa mara, hususani ikiwa ni kwa mwongozo wa Mungu, ndivyo utakavyoweza kupambanua zaidi ukweli upi ulikusudiwa kinyume na makosa ya mila za wanadamu zilizojiingiza.

Zaidi kuhusu jinsi vitabu vya Biblia vilivyokusanywa na kuwekwa pamoja na ni vipi vilikubaliwa kuwa ni maandiko matakatifu, haya yataongelewa katika masomo mengine.

Isome Biblia

Pale alipokuwa na njaa kimwili na akijaribiwa na Shetani, Yesu alinukuru toka kitabu cha Kumbukumbu la Torati:

“4 Mtu hataishi kwa mkate pekee, bali kwa kila neno linalotoka kwenye pumzi ya Mungu” (Mathayo 4:4).

Majibu yake mengine pia kwa Shetani vilevile yalitokana na kuyatumia na kuyanukuru Maandiko (Mathayo 4:7, 10) badala ya kutumia fikra za kibinadamu (ama mila zipinganazo za watu).

Sababu mojawapo juu ya ni muhimu kuisoma Biblia, ni kwa vile:

“3 Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima, ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia walimu makundimakundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli na kuzigeukia hadithi za uongo” (2 Timotheo 4:3-4).

Nyakati zilizokuwa zimelengwa hapo juu yaonekana ni hizi zetu na yamkini zitazidi kuwa mbaya.

Yesu alisali kwa Baba kuomba:

“17 Watakase na ile kweli yako. Neno lako ndilo kweli” (Yohana 17:17).

Zaburi inaeleza: “……Sheria yako ni kweli” (Zaburi 119:142b).

Kwa kuwa sheria ya Mungu na neno lake ndizo kweli, utawezaje kuujua ukweli pasipo kuisoma ama kuisikia Biblia ikisomwa kwako?

Kuisoma Biblia ndiyo njia ya kupima iwapo kitu fulani ni cha kweli. Biblia inatufundisha neno la Mungu na jinsi ya kuishi.

Paulo alikuwa mhubiri wa Mungu, lakini watu wangemjuaje? Wangelimjua kupitia uelewa wao wa Biblia.

Unaipataje elimu ya Biblia? Kwanza kabisa ni kwa kuisoma ama kusomewa. Kisha ni kwa kujifunza unayoyasoma ama kusomewa.

Pale Paulo alipohubiri kule Beroya ilitangazwa kwamba:

“11 Watu hawa walikuwa waungwana (yaani -waelekevu) kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, kisha wakayachunguza maandiko kila siku, waone ikiwa mambo hayo yalikuwa ndivyo hivyo” (Matendo 17:11).

Waberoya waliyachunguza Maandiko kila siku; yatupasa tufanye hivyo pia.

Maandiko yalivuviwa na Mungu (2 Timotheo 3:16) na wala hayakutokana na mawazo ya wale waliyoyaandika. Nabii zake zilitoka kwa Mungu, “Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu, bali wanadamu watakatifu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Takatifu” (2 Petro 1:21).

Ebu jionee yafuatayo toka maandiko ya Biblia:

“19 Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkilitii, kama taa ing’arayo mahala pa giza, mwafanya vema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu: 20 Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kutafsiriwa kama mtu fulani apendavyo tu.  21 Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu, bali wanadamu watakatifu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Takatifu” (2 Peter 1:19-21).

Neno la Mungu la unabii ni la hakika.  Hili kwa hakika ni faraja kwetu katika siku hizi za mwisho.

Zaidi ya kutupatia maagizo, mafundisho na kutuonya, kuisoma Biblia pia yaweza kukusaidia kuyajua mawazo na makusudi ya moyo wako:

“12Maana neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena linaukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo” (Waebrania 4:12).

Wakristo wanahitaji kuisoma Biblia na kujifunza.

Maelekezo Muhimu ya Mwisho

Sasa tuko tayari kuanza kipengele cha mwisho cha somo. Lakini subiri kidogo! Je, Biblia yako iko mbele yako? Ikiwa haiko, usiendelee kusoma hata neno moja zaidi! ISHIA HAPA KWANZA! NENDA na KAILETE BIBLIA YAKO.

Vilevile kalete karatasi kadhaa ama daftari, na kalamu ama penseli, ili uweze KUANDIKA NOTISI zitakazokusaidia kujifunza na kukumbuka.

Kozi hii itatumia tafsiri ya Biblia ya “New King James Version (NKJV)” kwa kuwa imekusudiwa ikupe tafsiri ya neno-kwa-neno na inatumia lugha ya Kiingereza kinachoeleweka kwa watu wa karne hii ya 21. Kwa masomo mengi yatakayofuata waweza kutumia aina ya tafsiri zingine, lakini maswali na majibu kimsingi yatatokana na NKJV labda tu pale pameelekezwa tofauti. Hivyo, kwa wengi wenu, tafsiri ya NKJV ya Biblia ndiyo chagua bora la kutumia katika Kozi ya Jifunze Biblia.

Sasa tuko tayari kulianza somo hili. KUMBUKA-UNAPASWA KUIFUNGUA Biblia yako KWENYE KILA AYA tunayokutajia katika somo hili. Usituamini sisi tu (timu iliyosimamiwa na marehemu C. Paul Meredith na/au Bob Thiel)—bali unapaswa uamini kile ambacho hasa Biblia inakifundisha.

Unapaswa USOME na KUSOMA, kwa kweli UJIFUNZE kila aya kwenye Biblia. Hii ni kozi ya KUJIFUNZA BIBLIA – kujisomea kuijua Biblia, na si tu kujifunza maneno tuliyoyaanisha hapa kwa ajili yako. Maneno yetu yamekusudiwa yakuelekeze ni wapi pa kutazama kwenye Biblia yako – ili kukusaidia uelewe namna ya kujifunza Biblia.

Sasa basi, pamoja na Biblia yako, kamusi (dictionary) nzuri, na karatasi zako za kuandika pointi zote zikiwa mbele yako, hii ndiyo mbinu utakayotumia kujifunza: Andika, kwa ufasaha, kwenye karatasi zako, Kichwa cha habari: “Somo la I,” na ukipigie mstari.

Kisha – “Mwisho wa Ulimwengu ni Nini?”

Chini yake, andika kila namba ya swali, kisha ANDIKA JIBU, kwa mwandiko wako mwenyewe (japo baadhi yenu mtapendelea kuchapa kwenye kompyuta ama kuandika kwenye simu zenu). Kama MFANO kwa maswali, hivi ndivyo utakavyo andika kwenye karatasi ama daftari lako:

1. Mathayo 24:3 – Hata alipokuwa ameketi {Yesu} kwenye Mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakisema, “Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa zama”.

Kadharika andika wazo ama taarifa zozote ziendanazo na swala hili unazohitaji kuzikumbuka. Utakapomaliza kuandika swali hili, na kujifunza majibu yake katika Biblia na kuwa na uhakika kwamba unalielewa, basi soma swali lifuatalo.

2. Andika majibu yako mwenyewe kwa swali, baada ya kuwa umeshasoma kile Biblia isemacho juu ya hilo kulingana na aya zilizoandikwa kuwa zinatoa majibu kwa swali hilo.

Baada ya swali la 3, andika majibu, na pia andika kila maneno ya aya ya Biblia, Mathayo 24:22.

Ikiwa waweza, itakuwa vema ukienda kwenye duka la stationary ama la vitabu na kujinunulia “punching Machine” ya kutobolea karatasi. Pia nunua file ama binder, ili uzitunze karatasi ama daftari la majibu na notisi zako pamoja na jarida hili la somo lenye maswali, yakiwa salama kwenye faili ama binder yako hiyo.

USITUTUMIE MAJIBU ya masomo haya. Yatunze tu kwa ajili ya kuyapitia na kujikumbusha. (Yawezekana tutatoa certificate ya bure kwa wale watakaokamilisha na kuhitimu kozi yote ama sehemu yake muhimu, lakini hili litaanza baada ya 2014, na kabla ya hapo tunatarajia kulitangaza hili kwenye mtandao na mahala pengine. Endapo tutafikia kufanya hivyo, tutakuomba ututumie nakala ya masomo uliyokamilisha na/ama maswali ya sehemu za kozi).

Wengine waweza kujiuliza, “Huku KUANDIKA ni kwa MUHIMU kweli?”

NDIYO!

Ni kwa MUHIMU MNO!

Kwa nini?

Hapa tunakupa sababu!

Tunapenda uielewe Biblia ki-ukweli. Wakristo wanatakiwa waje kuwa walimu (ona Waebrania 5:12) na hivyo wanatakiwa waijue Biblia yao vema ili: “Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu  awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu, lakini kwa unyenyekevu na upole” (1 Petro 3:15).

Kuyaandika yale unayojifunza kutakusaidia kukumbuka vema.

Zaidi sana, utaweza kufanya mapitio ya masomo yako kwa upesi zaidi, kila itakapohitajika, iwapo utakuwa umeyahifadhi katika mtindo huu. Kadharika, itakusaidia sana kuifafanua Biblia kwa wengine.

Sisi tunakupatia PICHA YA KWELI YA MUHTASARI WA BIBLIA. Siku zote utapenda kufanya mapitio ya masomo haya na KUTUMIA UFAFANUZI ULIOMO kuwaelezea wengine KWA MANENO YAKO MWENYEWE. Katika miaka ijayo kadri unapoyatumia maelekezo yaliyomo kuelewa na kuelezea pointi kadhaa za kwenye Biblia. Kumbuka, utahitaji kutumia angalau nusu saa kila siku katika kujifunza BIBLIA YAKO kupitia Kozi hii ya Kujifunza Biblia. Sasa tuko tayari….

Jifunze Biblia Yako: SOMO La 1

“Mwisho wa Ulimwengu” Ni nini?

1. Je, Yesu aliwahi kuulizwa juu ya janga linalotishia kwa sasa ustaarabu wa mwanadamu – MWISHO WA ZAMA HIZI na dalili za kurudi kwake? Mathayo 24:3.

2. Je, aya hii hapo juu inazungumzia kuhusu kuangamia kabisa na kufikia mwisho wa DUNIA YA ARDHI hii? – ama ilihusu kufikia MWISHO WA ZAMA ZA USTAARABU HUU wa utawala mbovu wa mwanadamu? Tafsiri za siku hizi za Biblia zinaitafsiri kwa usahihi namna gani Mathayo 24:3?

MAELEZO: Yapo maneno matatu ya Kigiriki yaliyovuviwa kutumika katika Agano Jipya ambayo yote yametafsiriwa kuwa ni “WORLD- Ulimwengu” katika Kiingereza cha “King James Version’ na kwa Kiswahili yalitafsiriwa kuwa ni “DUNIA”. Neno la awali la Kigiriki lililotumika kwenye Mathayo 24: 3 ni “aion”, kumanisha “AGE kwa Kiingereza” na kwa Kiswahili ”ZAMA”! – siyo dunia yaani ardhi tunayoishi juu yake. Kwa kuwa wengi wamekua wakisikia tafsiri zitokanazo na KJV zikisomwa mara kwa mara, wamepofushwa kwa kuelezwa maana isiyo sahihi juu ya kile Biblia inatoa unabii na kuamini kuwa ni mwisho wa sayari iitwayo dunia. Aya hii kamwe haizungumzii kuisha kwa maisha hapa duniani wala kuangamia kwa sayari yetu, bali ni juu ya kuisha kwa utawala wa kibinadamu wa kizazi hiki. Tafsiri ya Biblia ya NKJV imeliweka hili kwa usahihi (japo nayo, kama tafsiri zingine, inayo makosa sehemu zingine).

YESU, kwa hiyo, aliulizwa na wanafunzi wake juu ya kufikia mwisho kwa “zama” za kizazi hiki—kukoma kwa ustaarabu huu uliopo—na siyo kuteketea kwa sayari hii iitwayo dunia.

3. NI KIPI ambacho Yesu alitangaza kuwa KINGETOKEA IWAPO ASINGEREJEA? Mathayo 24: 22.

Alilolisema halihusiani na wokovu wa kiroho—bali ni kuokolewa toka kifo na maangamizi ya uharibifu utakaotokea. Tafsiri ya Moffatt imeliweka neno hili “asingeliokoka” kwa usahihi zaidi kwa kutafsiri: “HAKUNA NAFSI ingeokolewa IKIWA HAI.”

4. Je, Yesu anatoa unabii kwamba ni Wayahudi pekee, au ni Wakristo pekee, ndio watakaokabiliwa na janga hilo la kuangamia na kuteketea? Ama hapa anatoa unabii kwamba “HAKUNA MWENYE MWILI YEYOTE” angeokolewa toka janga hilo la uangamifu? Je, hili halithibitishi kuwa Mungu SHARTI aingilie kati ili kuzuia kuangamia kwa wanadamu wote?

5. Pale mataifa yatakapokuwa yanaangamizana katika MAJARIBIO YA KUMALIZANA ili kujipatia umilki wa ulimwengu, je, kujiingiza kwa Mungu KUTAZIFUPISHA siku za kusambaa kwa vita – vita ya dunia nzima? Linganisha Mathayo 24:22 na Marko 13:20.

MAELEZO: Aya hizi hazimaanishi kwamba Mungu atabadiri mpango wake wa ujumla wa siku zote wa maswala ya ulimwengu, bali kwamba, sawa na alivyopanga tangu awali, atajiingiza pale ambapo wanadamu watakuwa wamefikia muda wa kuangamizana wenyewe. Kulingana na mpangilio wake wa wakati wa kuingilia kati atakuwa amezipunguza SIKU ZA UTAWALA WA MWANADAMU juu ya watu, ambazo kama isingekuwa hivyo ingepelekea kuteketezwa kwa uhai wote wa mwanadamu.

Kwanini SHARTI Mungu Aingilie Kati

1. Je, kumewahi kuwepo kwa NYAKATI ZA TAABU zilinganazo na zile zitakazotokea mwishoni mwa zama hizi? Mathayo 24:21.

Je, Marko 13:19 inasema nini juu ya hili?

2. Je, kuna nabii yeyote ambaye naye aliwahi kutabiri juu ya kipindi hiki cha maangamizi? Yeremia 30:7, Danieli 12:1.

Sawa na kila ya aya hizi zinavyoeleza kuwa hakujawahi kuwepo hapo kabla, na wala hakutatokea tena, kipindi cha taabu kama hiyo, je, wanaweza kuwa kila mmoja anazungumzia kipindi cha matukio tofauti, ama wote wanataja juu ya KIPINDI KILEKILE KIMOJA CHAHITIMISHO la mambo mwhishoni mwa zama hizi?

3. Je, manabii wanatoa picha ya matukio ya kuogofya yatakayotokea mwishoni mwa zama hizi kuwa ni matokeo ya uharibifu mkubwa unaosababishwa na MBINU ZA KIVITA ZA KISAYANSI YA LEO? Yoeli 2: 1-3. Soma pia Isaya 33:11, 12.

Je kutakuwepo tena wakati kama huu? Ni kwanini unabii huu wa Yoeli unazungumzia kipindi kilekile sawa na unabii wa Yesu?—je, yawezekana ufukara uliozagaa sawa na ule anaouzungumzia Yoeli, waweza kutokea kutokana na mbinu mbovu na zilizopitwa na wakati za kivita?

4. Je, uangamifu na uharibifu waweza kutokea sababu ya kuwepo kwa silaha za atomic na MABOMU YA HYDROGEN, ROCKETS, SILAHA ZA KIBIOLOJIA, SILAHA ZA KIELECTRONIC, GESI ziangamizazo, na MBINU ZINGINE ZA KISASA ZA USAFIRISHAJI MAJESHI NA SILAHA ambazo zaweza kufutilia mbali ustaarabu wa mtu? Ufunuo 9:5-10 na 16-19.

Je, vielelezo hapa kwenye Ufunuo yawezekana zinaainisha mateso yatokanayo na gesi ya sumu na MAUAJI YA HALAIKI yatokanayo na silaha za kisayansi za kisasa? Yohana alikuwa AKIFAFANUA SILAZA ZA KIVITA ZA KIPINDI CHETU kwa kutumia VIELELEZO VYA ENZI ZAKE. Wakristo wa awali walijua hayo yalikuwa ni mafumbo tu kwa kuwa vitu vya aina hiyo havikuwepo kwa wakati huo. Ni dhahiri Yohana asingeweza kutumia maneno ya kileo kama vile “kifaru” au “rocketi” au “helicopter” au “jet” kwa sababau hakuna yeyote—wala hakuna mtafasiri yeyote—angeweza kuelewa inamaanisha nini.

5. Ebu kwa sasa tutafakari kwa ufupi juu ya wakati, kadri ya MIAKA 4300 ILIYOPITA, pale Mungu ALIPOINGILIA KATI maswala ya wanadamu ili KUAHIRISHA kile tukionacho kikitishia ulimwengu leo. Je, wanadamu walikuwa wanataka wajitengenezee umaarufu wa jina na kuufanya ulimwengu udumu katika muungano chini ya utawala wa kibinadamu? Mwanzo 11:4.

6. KWANINI Mungu aliingilia kati kwa kuzitawanya kabila za watu na kuziparanganya lugha za wanadamu kwenye mnara wa BABELI? Mwanzo 11:6.

7. Je, hili linaonyesha kwamba MUNGU AMEKUWA NA MPANGO katika kuahirisha na kuzuia maarifa ya ubunifu wa mtu? Je, si kwamba Mwanzo 11:6 pia inathibitisha kwamba pale wanadamu wafikiapo kuanza kutengeneza  utawala mmoja ulimwenguni, waanzapo kufikia kuanza kujifunza kuzungumza lugha za wenzao, na hatimaye KUWA NA USHIRIKIANO wa mali na MAARIFA ya kisayansi, hapo ndipo HAKUNA CHOCHOTE ambacho WANAWEZA KUZUIWA?—kiasi kwamba wataangamizana wenyewe kutokana na ubunifu wao?

CHANZO cha MATATIZO ya Ulimwengu

1. Kwa vile Mungu ataingilia kati ili kuzuia kuangamia kwa mwanadamu, kadharika vilevile atazuia vita visitokee tena kwa kuondoa kile kisababishacho vita! CHANZO HALISI CHA VITA ni nini? Yakobo 4:1-2.

2. Je, nia na fikra za ASILI YA MWANADAMU kimsingi ni njema ama ni zenye uovu? Linganisha Luka 11:13 pamoja na Warumi 3:10-19 pia na Mhubiri 7:29.

Elewa, kiujumla, kwamba asili ya mwanadamu ni MCHANGANYIKO WA WEMA NA UOVU. Yakobo 3:9-10 na Luka 6:45.

3. Je, ulimwengu huu ni mchanganyiko wa wema na uovu? Je, matendo na maamuzi yanayoonekana kuwa ni mema mbele ya viongozi wakuu na kwa watu kwa ujumla daima huishia kwenye matokeo ya kutisha? Methali 14:12.

Je, methali hii ni ya muhimu sana kiasi kwamba Mungu aliona ni vema aipe msisitizo kwa kuirudia kuitaja tena? Methali 16:25.

Je, si ukweli kwamba kukabiliwa kwa ulimwengu leo na kujiangamiza wenyewe INATHIBITISHA kwamba MSUKUMO WA ASILI ILIYO YA UOVU ya mtu UNANGUVU kuliko msukumo wa mtu wa asili ya wema?

4. Je, kiukweli MWANADAMU ANAIJUA NJIA YA KUIFIKIA AMANI? Warumi 3:17.

Nabii mmoja wa Agano la Kale aliuelezeaje uelewa wa wanadamu juu ya maswala ya amani? Isaya 59:8.

5. Katika ujinga, chuki na uoga wao, je, watawala wa ulimwengu walimuua Mfalme wa Amani (Isaya 9:6), Bwana wa utukufu? 1 Wakorintho 2:8.

6. NI NINI KINAMDANGANYA MWANADAMU aamini kwamba matendo yaishiayo kwenye mauti yataleta amani? Yeremia 17:9, 1 Yohana 2:16.

(Kumbuka kwamba katika Maandiko, moyo huzungumziwa kimafumbo kuwa ndio kituo cha akili ya mtu). Sasa je, watawala waweza kuwa wamedanganywa na TAMAA ZAO wenyewe waamini kuwa matendo yao maovu ni sahihi na yanafaa kwa ulimwengu?

Je, wanaweza kuwapotosha wanaowaongoza na kuchangia katika kuangamia kwao? Isaya 3:12, 9:16.

7. Je, PAULO ALITABIRI kwamba mwishoni mwa zama hizi, watu wangekuwa wasaliti, wavunja maagano, wenye uchu, watamanio mali na maeneo ya wenzao? 2 Timotheo 3:1-5.

8. Je, maarifa daima husababisha majivuno yaongezeke? 1 Wakorintho 8:1. Lakini upendo wa Mungu husababisha kitu gani? 1 Wakorintho 8:1.

Je, madaraka hupelekea mtu kuwa na majivuno? 1 Timotheo 3:6.

Kwa vile tunaishi katika zama za kuongezeka kwa maarifa ya kisansi, kitu kisababishacho watu wachache waweze kujikusanyia uwezo makubwa wa kiviwanda na kisayansi, je, asili ya mwanadamu itamfanya aweze kuzidi kuwa mwema na mwema zaidi ama MUOVU NA MUOVU zaidi katika siku za mwisho? 2 Timotheo 3:1,13.

9. Je, kwa sasa inawezekana, kupitia uwezo wa kisayansi na kitekinolojia, watu wenye uchu kutamani, kunyakua, na kuangamiza zaidi kuliko huko nyuma?

SHITUKA NA USAIDIE!-AMA UANGAMIE!

1. Je kutakuwepo wale WANAODHIHAKI katika siku za mwisho wakipinga kwamba Yesu hatarudi? 2 Petro 3:3, 4.

Pale mamlaka ya Mnyama itakapoinuka na kutambuliwa na Wanafiladefia waaminifu (Ufunuo 3:7-13) walio masalia ya Kanisa la Mungu, ambao watakuwa mbele katika kuitangaza Injili ya Ufalme kwa ulimwengu (Mathayo 24:14-15), je, hili litapelekea waingie kwenye mateso? Danieli 11:28-35.

Je, ustaarabu wa dunia utakabiliwa na janga la kuangamia kutokana na madikiteta vichaa? Mathayo 24:15, 22; Ufunuo 13.

2. Je, asili ya mwanadamu kimsingi imebadirika? Mathayo 24:37-39 na Luka 17:26-30.

Ijapokuwa kimsingi asili ya mwanadamu haijabadirika kuanzia siku za Nuhu, je, njia za kisayansi za kuangamizana zimebakia zilezile? Je, mataifa yanazidi kubuni na kuunda mamlaka kuu na KUU ZAIDI za kuleta amani? — ama ni kwa ajili ya MAANGAMIZI YA HALAIKI?

3. Je wengi wa watu leo WANAHANGAISHWA na tishio la mauti litokanalo na vita vya maangamizi kugombea kuutawala ulimwengu? 2 Wathessalonike 2:9-12, Mathayo 24:39.

Je, watu WAMEAMUKA vya kutosha juu ya matukio ya ulimwengu au hata tu kuyatarajia? Je, ULIMWENGU unaendelea na mambo yake ya kila siku PASIPO KUJALI WALA KUSIKIA KILE KINACHOENDA KUTOKEA?

4. Je, jitihada za kibinadamu katika kuelimisha ulimwengu na mipango ya amani itazuia uteketezwaji? Isaya 33: 7-8.

Pale mabalozi wa amani watakapokuwa wakilia kwa uchungu—wakati miji imeteketezwa—je, hapo ndipo MUNGU ATAINGILIA KATI ili kuwaokoa wanadamu? Aya ya10.

5. Kote katika Biblia, vita inaonyeshwa kuwa ni malipo ya dhambi—iletwayo kama matokeo ya uchu ama tamaaa mbovu. Yakobo 4: 1-2.

Je, mabalozi wa mataifa wanaweza kusamehe dhambi? Je, wanaouwezo sasa wa kusitisha VITA kabisa ikome milele, ambayo ndiyo malipo ya uovu wao?

MAELEZO:  Amani ya ulimwengu haiwezi kuja hadi ADHABU ya dhambi isamehewe kwa malipo sitahiki. Ni dhahiri NI KRISTO PEKEE NDIYE AWEZAYE KUSITISHA VITA VYOTE kwa vile ni yeye pekee ndiye aliyelipa malipo kamili—kifo—kwa ajili ya dhambi. Kristo alikufa ili sisi sote tusiweze kufa wakati wa maangamizi ya kutisha yajayo. Mungu ataisitisha adhabu juu ya familia ya wanadamu kwa kujiingiza mapema katika maswala ya wanadamu. Mwanae tayari alijitoa akaitwaa adhabu ya mauti, akafa badala yetu.

6. Baada ya kuingilia kati, JE, MUNGU ATAANZISHA ELIMU KWA ULIMWENGU NA KUONDOLEA MBALI CHANZO HALISI CHA VITA? Isaya 2:3-4 na Mika 4:1-4.

Badala ya kufundishwa sawa na taasisi za leo za kielimu namna ya kuunda vyombo vya kivita vya kuwaangamiza wanadamu wenzao, je, watu WATAFUNDISHWA kujizuia na kupewa NIDHAMU BADALA YA ASILI YA KIBINADAMU – ili kuiongoza busara ya ubunifu—iunde vyombo vya uzalishaji wa kiamani?

7. Je, MATAIFA muda huo yatahitaji KUKEMEWA kwa nguvu ya kimamlaka kuu? Isaya 34:2.

Je, wataelimishwa juu ya njia sahihi ya maisha—njia iletayo amani? Isaya 30:21.

Hili ndilo swala ambalo Wakristo katika zama hizi watakuwa wakisaidia kulitimiza. Hii ndiyo sababu nyingine ya umuhimu wa wewe kuisoma na kujifunza Biblia kwa sasa.

8. Je, neno la unabii ni la kuaminika? 2 Petro 1:19-21.

Je hili si faraja pale tuonapo mengi ya yanayoendelea katika ulimwengu leo?

 

 

 

 

Posted in Kiswahili
About CCOG
The Continuing Church of God, which attempts to represent the most faithful remnant of the Philadelphia (Revelation 3:7) portion of the Church of God, bases its beliefs on the Holy Bible. Read CCOG's statement of beliefs for more information.