Vipengele vya Imani vya Kanisa la Continuing Church of God

STATEMENT OF BELIEFS OF THE CONTINUING CHURCH OF GOD (KATIKA LUGHA YA KISWAHILI)

Vipengele vya Imani vya Kanisa la Continuing Church of God

 “…muishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu” (Yuda 3); “Upendo wa ndugu (Filadefia) na udumu (Waebrania 13:01); ”…wakidumu katika mafundisho ya Mitume” (Matendo. 2:42).

Madhumuni ya makala hii ni kuorodhesha vipengele mbalimbali wanavyoamini wale walio sehemu ya mabaki ya kipindi cha Filadefia cha Kanisa la Mungu, na zaidi sana Kanisa la Continuing Church of God (bado havijakamilika). Na kwa kuwa Wana-filadelfia wametawanyika miongoni mwa makundi/maeneo mbalimbali, baadhi ya Wana-filadefia wanaweza wasiwe wanaamini vipengele vyote vya imani vilivyomo katika makala hii, lakini watakukubaliana na vingi miongoni mwake (Jisomee zaidi juu ya Imani za makundi mengine kupitia: Articles on various COG groups). Lakini wale walio waumini wa Kanisa la Continuing Church of God wanaamini na kushika vipengele hivi vyote.

Kanisa la Continuing Church of God lilitangazwa rasmi mnamo 28 Disemba 2012, hususani kwa kuwa kufikia tarehe hiyo ilikuwa imebainika wazi kwamba kulikuwa hakuna kundi linguine la makanisa ya Mungu (COGs) lililokuwa bado limeshika na kujitoa kwa mafundisho ya kipindi cha Filadefia ama lilikuwa bado na “upendo wa ukweli” wa kutosha.

Mafundisho na Imani ya Kipindi cha Efeso na Smirna

Kitabu cha Ufunuo ni kitabu cha kinabii: “Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu ili awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi” (Ufunuo 1:1). Hivyo, nyaraka kwa Makanisa ya Ufunuo 2 & 3 sharti zieleweke kiunabii. Kadharika, vipengele kadhaaa vya nyaraka hizo VILIPASWA ziwe ni kwa wakati ujao na si kwa ajili ya nyakati ambazo Yohana aliandika ujumbe huo.

Ukifuatilia historia ya Kanisa la Kikristo kupitia makanisa saba ya Ufunuo 2 & 3 utakuta vielelezo muhimu vionyeshavyo ni nani ndio uzao wa kweli wa kanisa la kweli leo (Kwa maelezo zaidi, tafadhali soma makala iitwayo: The Churches of Revelation 2 & 3). Ufuatiliaji huu unatoa taarifa ionyeshayo kwamba Kanisa la kweli la Mungu (COG) siyo la Kiprostanti (Protestant) wala la Kiorthodoxi (Eastern Orthodox) ama la Kikatoliki (Roman Catholic), bali badala yake ni lile kanisa ambalo linashika na kuamini kwelikweli imani ileile sawa na mitume wa mwanzo. Na pamoja na wengi wajiitao kuwa waumini wa Ukristo kudai kuwa wanayo imani ya Yesu na ya mitume wake wa awali, wengi wao hata hawafahamu ni vipengele vipi vya Imani ambavyo mitume wa awali na wale waaminifu waliofuatia baada yao hasa waliamini na kushika!  Biblia inaonyesha wazi kwamba Yesu hutembea katikati (miongoni) mwa makanisa haya saba (Ufunuo 1:9-13), hii ikionyesha kuwa makanisa haya saba yanawakilisha vipindi mbalimbali vya kanisa. Ukweli kwamba kuna makanisa saba yaliyotumiwa nyaraka na kwamba namba saba inaashiria ukamilifu, ukizingatia pia ukweli kwamba makanisa haya yametajwa katika mfuatano uleule wa miji ya njia ya barua ya kipindi cha Milki ya Rumi, inakubaliana na mtazamo kwamba makanisa haya yangewakilisha hali ya kanisa la kweli katika vipindi vyake vyote katika mfuatano uleule.

“Vipindi” viwili vya kwanza vya Kanisa la Mungu (na makanisa ya kwanza mawili yaliyoanza kutajwa katika Ufunuo) vilikuwa ni vile vya Efeso na Smirna na vilianzia siku ya Pentekoste katika Matendo 2 (kuanzia mwaka 31 B.K.) hadi kufikia katikati ya karne ya tano (ambapo wafuasi wake wakati mwingine walijulikana kwa walionje kama “Wanazarayo” (Nazarenes)–Kanisa la Continuing Church of God linafuatilia mwanzo wake hadi kwa Wanazarayo wa awali wa karne ya kwanza hadi ya tano).

Jionee mafundisho yafuatayo ya Wakristo wa awali ambayo taarifa za kihistoria zinaonyesha yalishikwa na kufundishwa na kanisa wakati wa vipindi vya Kanisa la Efeso na/ama la Smirna–ambayo yote miongoni mwake ndiyo yanayokubaliwa na kufundishwa na Kanisa la Continuing Church of God, wakati ni sehemu yake kidogo tu ndiyo hukubaliwa/hufundishwa/bado inashikwa na Wakatoliki, Waprostanti na Waorthodoxi (Roman Catholics, Orthodox, or Protestants ingawa viongozi wao wa awali ambao Wakatoliki wanawaheshimu kama  “Watakatifu” wao pia waliyashika):

Ubatizo wa Wakristo (Baptism of Christians) ulikuwa ni kwa kuzamishwa kwenye maji mengi na haukuhusisha watoto wachanga.

Biblia yote kamili (Bible) ikiwa ni Agano la Kale (Old Testament) na Agano Jipya (New Testament) yote ilishikwa na Kanisa la kweli la Asia Ndogo.

Mtazamo wa Kibinitaria (A Binitarian View) unaoamini katika Mungu Baba na Mwana huku ukiamini Roho Takatifu kuwa ni “Uweza”—Nguvu toka kwa Mungu ndio ulioaminiwa na viongozi wa Kikristo wa kweli wa kipindi cha Mitume na waliofuatia kipindi hicho.

Sherehe za kuzaliwa (Birthdays) hazikuazimishwa na Wakristo wa awali.

Kuzaliwa Mara ya Pili (Born-Again) ilimaanisha ni kuzaliwa wakati wa ufufuo, na si wakati wa kuongoka.

Kutooa/Useja kwa Maaskofu, Wachungaji na Watawa (Celibacy for Bishops/Presbyters/Elders) haikuhitajika.

Uongozi katika Kanisa (Church Governance) ulitokea juu kwenda chini, si kwa kura.

Sherehe ya Kuzaliwa Mwokozi (Christmas) haikuwahi kusherehekewa na yeyote miongoni mwa Wakristo waliokuwepo kabla ya karne ya tatu, wala na yeyote miongoni mwa wale walioshikilia imani ya awali.

Tohara (Circumcision), japokuwa haikuwa ni lazima, kwa muda mrefu ilitekelezwa na Wakristo wa awali wa Kinazarayo.

Maungamo ya dhambi (Confession of sins), hayakufanyika kwa wachungaji na kitubio hakikuhitajika.

Wakristo kuvaa Uungu (Deification of Christians), (ambako kutaanza mara baada ya Ufufuo wa Kwanza) ilikuwa ni imani iliyofundishwa na viongozi wa mwanzo wa Kanisa.

Majukumu rasmi ya Wachungaji/Wazee wa Kanisa (Duties of Elders/Pastors) yalikuwa ni ya kiuchungaji na kiuelimishaji (Pastoral and Theological), siyo ya utoaji sakramenti–wala hawakutakiwa kuvaa kama wengi wavaavyo leo.

Sikukuu iitwayo leo Easter haikuwahi kuadhimishwa wakati wa Kanisa la enzi za Mitume.

Sikukuu Takatifu za vipindi vya vuli na kipupwe (The Fall and Spring Holy Days) ziliadhimishwa na Wakristo wa kweli wa awali.

Baba (The Father) alitambuliwa kuwa ni Mungu na wote waliokuwa Wakristo wa awali.

Injili ya Kweli (The True Gospel) ilihusu Ufalme wa Mungu pamoja na utii kwa sheria ya Mungu na ndivyo walivyoielewa waumini wa mwanzo.

Mbingu (Heaven) haikuwahi kufundishwa kuwa ndiyo tuzo ya Wakristo.

Roho Takatifu (Holy Spirit) haikuwahi kutajwa kuwa nayo ni Mungu ama ni nafsi nyingine ya Mungu enzi za Wakristo wa kweli wa awali.

Nyimbo za ibadani (Hymns) maranyingi zilitokana na Zaburi, wala siyo sifa kwa Kristo.

Kuabudu “Sanamu” (Idols) ilikatazwa na kufundishwa kuwa ni dhambi, ikiwemo kuabudu msalaba.

Roho ama nafsi kutokufa (Immortality of the soul) haikuwahi kufundishwa.

Yesu Kristo (Jesus) aliaminiwa na Wakristo wa kweli kuwa ni Mungu.

Ufalme wa Mungu ujao hivi karibuni hapa duniani (The Kingdom of God) ulihubiriwa.

Uondoaji wa “Chachu” (Leavened Bread) ulifanyika Katika nyumba za Wakristo wa awali katika muda ambapo Wayahudi nao walifanya hivyo.

Kipindi cha “Mfungo wa Majivu” (Lent) hakikuwa kinaadhimishwa na kanisa la awali.

Wafu kukaa “Tohorani” (Limbo) haikuwahi kufundishwa na kanisa la awali.

Maria (Mariamu)(Mary) alieleweka kuwa alikuwa mama wa Yesu, aliyepewa neema (Luka 1:28) na pia aliyebarikiwa (Luka 1:48), lakini kamwe Wakristo wa awali hawakuwa wanamwabudu wala kumuomba,n.k.

Kujiunga na Majeshi (Military Service) ilikuwa hairuhusiwi kwa Wakristo wa kweli wa awali.

Umillenia (Millenarianism) – (Utawala wa Kristo wa Miaka elfu hapa duniani uitwao “Millenia”) ulifundishwa na Wakristo wa awali.

Watawa kuishi kwenye majumba maalumu (Monasticism) haikuwahi kusikika enzi za Kanisa la awali.

Pasaka iitwayo (Passover) iliandhimishwa kila mwaka kwenye siku ya 14 ya mwezi Nisan wakati wa Kanisa la enzi za Mitume na pia wakati wa Wakristo wa karne ya pili kule Asia Ndogo.

Sikukuu ya Pentekoste (Pentecost) iliadhimishwa kwenye siku ya Jumapili (Siku ya Kwanza ya Juma) miongoni mwa Wayahudi, na ndivyo Wakristo wa awali walivyoiadhimisha.

Wafu waovu kukaa kwa muda “Toharani” (Purgatory) ili kufanya kitubio haikuwahi kufundishwa na Kanisa la awali la enzi za Mitume.

Kufufuliwa kwa wafu wote (The Resurrection) ilifundishwa na Wakristo wa kweli wa Kanisa la awali.

Siku ya Sabato (The Sabbath) iliadhimishwa kila Jumamosi na Kanisa la enzi za Mitume na wakristo waliofuatia enzi hiyo.

Iliaminiwa na kufundishwa kwamba, Wokovu (Salvation) umetolewa kwa “Wateule pekee”kwa sasa, ambapo waliosalia wataitwa baadaye; japo si wote miongoni mwa Wakristo wa awali walioamini na kufundisha hivyo (wapo ambao pia hawakuwa na uelewa sahihi) kwani si wote walitekeleza agizo: “…muishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu” (Yuda 3).

Mpango wa Mungu wa miaka elfu sita ya mwanadamu kujitawala mwenyewe (God’s Six Thousand Year Plan) uliaminiwa na kufundishwa na Wakristo wa awali.

Jumapili (Sunday) haikuwa siku ya ibada wala haikuwahi kuadhimishwa na Wakristo wa enzi za Kanisa la Mitume ama wale waliowafuatia enzi hiyo.

Amri kumi za Mungu (The Ten Commandments) zilishikwa na Wakristo wa enzi za Mitume na enzi iliyofuatia tena ni katika mfuatano unaoenezwa na Kanisa la Mungu (COG) leo.

Zaka na Sadaka (Tithes and Offerings) zilitolewa na waumini ili kuendesha huduma ya kazi ya Mungu katika kuhudumia wachungaji, kazi za kanisa, wahitaji, uinjilisti na kuhubiri.

Mila (Tradition) zilileta athari fulani kwa Wakristo wa enzi za karne ya pili, lakini kamwe hazikuwahi kuwa tegemoe kuliko Biblia Takatifu.

Utatu Mtakatifu (The Trinity) lilikuwa ni neno ambalo halikuwahi kutumiwa na Mitume ama na Wakristo wa karne ya pili kufafanua “Uungu”, japo kuna utatu Fulani uliotambuliwa.

Vyakula “Najisi” (Unclean Meats) vililiwa na wengi miongoni mwa “Waallegoria”, lakini kamwe havikuliwa kabisa na Wakristo wa kweli.

Uzao wa Bikira (The Virgin Birth) ulikubaliwa na kufundishwa na Wakristo wa kweli wote waliokuwa kinyume na Mkutano wa Nikea.

Kanisa la Continuing Church of God linaendelea kufundisha yote yaliyofafanuliwa hapo juu sawa na yalivyokuwa yakifundishwa na Mitume wa Kristo wa awali na pia na wale waliofuata bada yao.

Kanisa la Continuing Church of God hali kadharika linafuatiria lilikotoka na kukuta kwamba ni uzao wa mitume wa awali kama Petro (Peter), Paulo (Paul), na Yohana (John) kupitia kwa wafuasi wao waaminifu kama Polycarp, Polycrates, pamoja na viongozi/maaskofu wengine wanaojulikana wa kipindi cha mwanzo waliokuweko kule Asia Ndogo hadi mapema karne ya tatu, ambako viongozi wake kumbukumbu zao kufikia hadi mwaka 135 B.K. zinajulikana katika Yerusalemu, na taarifa za kanisa na uongozi wake kwa Antiokia kama vile Serapio (Serapion) uliokuwepo kufikia hadi 211 B.K. nazo bado zinaeleweka. Wakati Petro ndiye aliyekuwa kiongozi miongoni mwa mitume, baada ya kifo chake, majukumu hayo ya uongozi yalihamia kwa mtume mwingine (Yohana) na si kwa mzee wa kanisa kama yule aliyekuwa akiishi Rumi kama wengine wanavyodai.

Mafundisho ya enzi za Filadefia ni yapi?

Pamoja na kwamba Kanisa la Mungu daima lilijitahidi kuing’ang’ania imani, kadri mda ulivyopita, baadhi ya mafundisho yalipotea na Kanisa la enzi za Sardi za Kanisa la Mungu lilipoteza kweli nyingi (Ufunuo 3:1-3).

Kweli zifuatazo ni baadhi ya mafundisho yaliyorejeshwa kwa Kanisa la Mungu wakati wa kipindi cha Kanisa cha Filadefia baada ya Kanisa la kipindi cha Sardi kuwa limeyapoteza:

1. Injili ya Kweli (Makala yenye maelezo yanayofafanua zaidi ni pamoja na The Gospel of the Kingdom of God was the Emphasis of Jesus and the Early Church).

2. Kusudi la Mungu (Makala yenye maelezo yanayofafanua zaidi ni pamoja na Deification: Did the Early Church Teach That Christians Would Become God?).

3. Mpango wa Mungu Kupitia Sikukuu Takatifu (Makala kadhaa zenye maelezo yanayofafanua zaidi ni pamoja na Is There “An Annual Worship Calendar” In the Bible? Passover and the Early Church, na Did Early Christians Observe the Fall Holy Days?).

4. Uongozi Sahihi wa Kanisa (Makala mbili zenye maelezo yanayofafanua zaidi ni pamoja na The Bible, Polycarp, Herbert W. Armstrong, and Roderick C. Meredith on Church Government na Polycarp’s Letter to the Philippians).

5. Mungu ni nani na ni Nini? (Makala yenye maelezo yanayofafanua zaidi ni pamoja na One God, Two Beings Before the Beginning).

6. Mtu ni Nani na ni Nini? (Makala mbili zenye maelezo yanayofafanua zaidi ni pamoja na What is the Meaning of Life? and Did Early Christians Believe that Humans Possessed Immortality?).

7. Roho ndani ya Mtu (Makala yenye maelezo yanayofafanua zaidi ni pamoja na Did Early Christians Believe that Humans Possessed Immortality?).

8. Malimbuko (Mazao ya Kwanza) Katika Enzi hizi (Makala yenye maelezo yanayofafanua zaidi ni pamoja na Pentecost: Is it more than Acts 2?).

9. Elimu juu ya Millennia Hasa ni Nini (Makala yenye maelezo yanayofafanua zaidi ni pamoja na Did The Early Church Teach Millenarianism and a 6000 Year Plan?).

10. Ukweli kuhusu Roho Takatifu (Makala yenye maelezo yanayofafanua zaidi ni pamoja na Did Early Christians Think the Holy Spirit Was A Separate Person in a Trinity?).

11. Wakristo kwa Sasa Wametungwa Mimba (Makala yenye maelezo yanayofafanua zaidi ni pamoja na Born Again: A Question of Semantics?).

12. Kuzaliwa-Tena kwenye Ufufuo (Makala yenye maelezo yanayofafanua zaidi ni pamoja na Born Again: A Question of Semantics?).

13. Kuitambua Israeli ya Kimwili (Makala yenye maelezo yanayofafanua zaidi ni pamoja na Anglo – America in Prophecy & the Lost Tribes of Israel).

14. Jinsi Kuitambua Israeli Kunavyofungua Uelewa Sahihi wa Nabii za Biblia (Makala yenye maelezo yanayofafanua zaidi ni pamoja na Anglo – America in Prophecy & the Lost Tribes of Israel).

15. Zaka ya Pili na ya Tatu (Makala yenye maelezo yanayofafanua zaidi ni pamoja na Is Third Tithe Still Valid Today?)

16. Kuitambua Babeli na Binti zake (Makala tatu zenye maelezo yanayofafanua zaidi ni pamoja na Europa, the Beast, and Revelation, Which Is Faithful: The Roman Catholic Church or the Genuine Church of God?, and Hope of Salvation: How the Genuine Church of God differ from most Protestants).

17. Ibilisi kaudanganya Ulimwengu Wote (Makala yenye maelezo yanayofafanua zaidi ni pamoja na The Day of Atonement–Its Christian Significance).

18. Tunapaswa Tujitenge (Makala mbili zenye maelezo yanayofafanua zaidi ni pamoja na Why Be Concerned About False and Heretical Leaders? na Overview: How Does the Church of God Agree and Disagree with Other Faiths Professing Christ?)

Pasipo kuzama katika maelezo zaidi hapa, makala za karne ya pili za Theophilo wa Antiokia, kwa mfano, zinaainisha kwamba Wakristo waliamini wangezaliwa mara ya pili wakati wa ufufuo (Theophilo wa Antiokia. Kwa Autolycus, Kitabu cha 2, Sura XV) pamoja na maandiko mengine ya awali vinathibitisha kwamba walikuwepo wale waliokuwa wakimkiri Kristo baada ya mitume wa mwanzo kufariki ambao wanaonekana kuwa waliamini kweli hizi zilizoorodheshwa hapa ambazo “zimerejeshwa baada ya kuwa zimepotea”. Wakristo wa asili ya Kiyahudi wa kipindi cha karne ya kwanza B.K. yaonekena walikuwa na uelewa juu ya angalau baadhi ya kule Israeli ya kimwili walikokuwa na walijitahidi kuipeleka habari ya Injili huko (mfano Yakobo 1:1).

Kimsingi, Wanafiladefia, tofauti na wengine wanaodai kuwa nao wametokana na Kanisa la Mungu (COG), wao waliweka mkazo mkubwa kwenye upendo wa kifiladefia kwa kusaidia kuitimiza Mathayo 24:14 pamoja na maeneo mengine ya Maandiko yaagizayo kuipeleka Injili, huku wakitambua ukweli kwamba Mungu hutenda kazi kupitia kwa viongozi aliowavuvia na mara zote amekuwa na kiongozi wa ngazi ya Kiinjilisti ama juu zaidi akiwa ndiye msimamizi wa kipindi cha Filadefia, na hadi sasa anaendelea kutenda hivyo kupitia kwa kundi dogo la masalia ya enzi hiyo lililopo leo.

Baadhi ya Imani kwakina

Kanisa la Continuing Church of God, ambalo linajitahidi kuwawakilisha masalia ya wanafiladefia wachache waliobaki miongoni mwa Kanisa la Mungu, limejikita kwenye Biblia ambako ndiko linatoa imani yake. Baada ya kifo na kufufuka kwa Yesu Kristo, mafundisho yetu, taratibu, sera na destruri zetu zimebaki kujikita kwenye mizizi ya Kanisa la awali la Yerusalemu (Matendo 2, Mwaka 31 B.K.), pamoja na kwa Wakristo waaminifu wa Antioki na Asia Ndogo wa karne ya kwanza (Kama vile Mtume Petro, Paulo, na Yohana) na ya pili B.K. (viongozi kama vile Polycarpo, Thaseas, Serapion, na Polycrates). Hawa wafuasi wao wengi walisambaa ulimwenguni kote  wakifungua makusanyiko ya waumini (congregations) katika nyakati zote.

Yesu Kristo alifundisha kwamba kanisa la kweli lingebaki kuwa “kikundi kidogo” (Luka 12:32), lingechukiwa na ulimwengu (Mathayo 10:22), na litateswa (Mathayo 10:23). Vilevile, alifundisha kwamba, wakati wa kipindi hiki, ni wachache tu ndio wangeipata njia ya kuingia kwenye uzima wa milele (Mathayo 7:14; 20:16). Mtume Yuda anaashiria ukweli kuwa idadi ya watakatifu ilikuwa ndogo sana (Yuda 14), wakati huohuo Mtume Paulo naye aliliita kanisa la Mungu lililo dogo kuwa lilikuwa ni “masalia” (Warumi 11:5).

Zaidi ya hapo, Biblia inaonyesha kuwa kanisa la kweli lisingebakia kuwa na makao yake makuu katika mji mmoja peke yake kwa mda wa karne zote za historia yake (Waebrania 13:14; Mathayo 10:23), hivyo kwa kuuelewa ukweli juu ya makanisa ya Ufunuo sura ya pili na tatu na ni vipi Kanisa la Mungu lenyewe lilivyodumu inasaidia kulitambua Kanisa la Mungu katika maeneo mbalimbali.

Katika karne ya 20, enzi za kipindi cha Filadefia cha Kanisa la kweli (Ufunuo 3:7-13) ndipo kilipoanza. “Enzi” hii kimsingi ilianza kuwakilishwa na Radio Church of God ya kale ambayo baadaye ilibadilishwa jina na kuitwa Worldwide Church of God WCG) na mwanzilishi na kiongozi wake marehemu Herbert W. Armstrong. Pamoja na kuonekana kwamba “enzi” hii ilifikia mwisho mara baada ya kifo chake, masalia ya enzi hii ya Filadefia ya waumini walio waaminifu bado yapo na ndiyo kwa sasa walionakinara cha kazi ya Mungu, na wataendelea kudumu hadi mwisho wa enzi ya kanisa (Ufunuo 3:10-11; 12:14-17a). Kanisa la Continuing Church of God, lenye makao makuu yake hapa duniani kwenye eneo la Miji Mitano ya California (katika mji wa Arroyo Grande), linajitahidi kuiwalisha kondoo walioko mahala pote duniani katika nyakati hizi za karne ya 21.

BIBLIA TAKATIFU

Biblia Takatifu ni Neno lenye uvuvio wa Mungu. Kulingana na mgawanyiko wake sahihi, ni mkusanyiko wa vitabu 66, ambapo vitabu 39 vinatokana na maandiko ya Kiebrania – Agano la Kale (The Old Testament Canon) na 27 ni vitabu vinavyotokana na maandiko ya Kigiriki-Agano  Jipya (The New Testament Canon). Maandiko haya yamevuviwa na yanabeba elimu ya kile kinachohitajika ili kupata wokovu (2 Timotheo 3:15-17; Mathayo 4:4; 2 Petro 1:20-21). Neno la Mungu ni kweli (Yohana 17:17) na hayawezi kukosea wala kushindwa kutimia ikiwa hayajabadirishwa toka uasilia wake (Yohana 10:35).

MUNGU NI ROHO, MUNGU NI UPENDO

“Mungu ni Roho, na wamwabuduo halisi inawapasa kumwabudu katika roho na kweli” (Yohana 4:24). Njia za Mungu ziko juu kuliko mawazo ama njia za wanadamu (Isaya 55:9). “Mungu ni upendo” (1 Yohana 4:8,18); kujua zaidi jisomee makala yetu: (The Ten Commandments Reflect Love, Breaking them is Evil). Roho Takatifu inakaa ndani ya Mungu Baba na ndani ya Mungu Mwana, na kutoka kwao husambaa na kujaa kote mbinguni, angani na duniani (Wafalme 8:27; Zaburi 139:7; Yeremia 23:24).  Mpango wote kamili wa Mungu kwa wanadamu unatokana na upendo.

UUNGU

Baba na Mwana kwa pamoja wanakamilisha Uungu (Warumi 1:20; Wakolosai 2:9) na hutenda yote kupitia Roho yao Takatifu. Maandiko yaonyesha kuwa Mungu ni Familia moja ya kiuweza na ya milele inayoundwa na wawili kwa sasa, Mungu Baba na Neno (Mungu Mwana) (Mwanzo 1:26; Waefeso 2:19; 3:14-15; Yohana 1:1,14), ambapo hapo baadaye watoto waaminifu nao wataongezwa katika familia hiyo (Waebrania 2:10-11, 1 Yohana 3:1-2; Waefeso 3:14-15) nao pia watafanyika sawa na Yesu Kristo (Warumi 8:29), ambaye naye ni Mungu (Yohana 1:1-3,14, 20:28-29; Wakolosai 2:9). Roho Takatifu siyo mungu mwingine na hutolewa kama msaada kwa wale waliotubu kiukweli na kubatizwa (Matendo 2:38-39). Wakristo wa awali waliokuwa waaminifu waliamini juu ya uungu unaoundwa na Mungu Baba na Mungu Mwana, ujulikanao kama “Godhead binitarian view”.

UTAWALA WA KIBIBLIA

Yesu alifundisha, “Baba yangu ni mkuu kuliko mimi” (Yohana 14:28) wakati pia mtume Paulo naye alifundisha “Kichwa cha Kristo ni Mungu” (1 Wakorintho 11:3), hivyo mamlaka ya juu kibiblia ni Mungu Baba. Baada ya hapo, tunakuta kwamba “Kristo ni kichwa cha Kanisa” (Waefeso 5:23) na “Ni Neno” (Yohana 1:14), hivyo hakuna kiongozi yeyote wa kidini wa kibinadamu anayeruhusiwa kufundisha ama kutoa maagizo yapinganayo na Neno la Mungu – Biblia ambalo ni Kristo (Ona Marko 12:13-27; Matendo 5:29).

Utaratibu wa kiuongozi unaoanzia juu kuja chini (hierarchical) ndio unaofundishwa katika Agano Jipya (1 Wakorintho 12:28) na unaonyeshwa kuwa ndio ulio sahihi kwa kanisa (Waefeso 4:11-16).  Mfuatano sahihi ukiwa kwamba, chini ya Yesu Kristo wanafuata Mitume, kisha Manabii, kisha Wainjilisti, wakifuatiwa na Wachungaji, baadaye Walimu (Waefeso 4:11).

Kuanzia enzi za Pentekoste nyakati za Matendo ya Mitume (Matendo 2:1-4), watumishi wa Mungu wameteuliwa kwa kuwekewa mikono kutoka miongoni mwa wale walioonekana kuwa wamejazwa Roho Takatifu, kuanzia na mitume (Matendo 9:17; 2 Timotheo 1:6) na pia kupitia kwa wale ambao walikuwa tayari walishawekewa mikono na kufanyika watumishi wa Mungu. Wakati Wakristo wanapaswa kuwatii daima katika Bwana viongozi wao wa kiroho (Waebrania 13:7, 17), viongozi hawa nao wanapaswa kuongoza wakifuata kanuni za kibiblia (1 Timotheo 3:1-12; Waebrania 13:17) na kuongoza wakimuiga Kristo ambavyo yeye ndivyo angetaka waongoze (Mathayo 20:25-28).

WAKRISTO WANAPASWA KUDUMU KATIKA PENDO LAKE

Upendo ndivyo Mungu aliovyo (Yohana 3:16; 1 Yohana 4:8, 18), Amri zake (Mathayo 22:37-40), pamoja na njia yake ya maisha (Yakobo 2:8-11; 1 Yohana 5:3) vyote ni upendo. Wakristo huzishika amri zake na kudummu katika upendo wake (Yohana 15:9-10; 1 Yohana 2:3-6). “Sasa kupitia hili tunajua kuwa twamjua yeye, ikiwa twazishika amri zake. Yeye asemaye, “Ninamjua,” lakini hazishiki amri zake, ni muongo, wala kweli haimo ndani yake. Lakini yeye alishikaye Neno lake, ni dhahiri pendo la Mungu limekamilika ndani yake. Na kwa hili ndipo tuwezapo kujua ikiwa kweli tuko ndani yake. Yeye asemaye anakaa ndani yake yampasa yeye pia aenende sawa na yeye alivyotembea” (1 Yohana 2:3-6). Wakristo wanapaswa “kumuiga Krristo” (1 Wakorintho 11:1). Pamoja na kuzishika sheria za Mungu na kuishi katika njia ya upendo ya utoaji; wakristo vilevile wanatakiwa: wasali mara kwa mara (1 Wathesalonike 5:17), Wajisomee Biblia mara kwa mara (Matendo 17:11; 2 Timotheo 2:15), watafute muda wa kumtafakari Mungu na Biblia (Wafilipia 4:8), na, wale ambao miili yao inawaruhusu, wafunge kila iwezekanapo (Mathayo 6:16-17).  Wakristo wanapaswa kuishi kwa upendo kwa wengine (Mathayo 22:36-40) na wawe na huruma (Luka 6:36).

Ukweli ni kwamba Biblia na ujumbe wake kiukweli inahusu upendo—upendo kwa Mungu na upendo kwa wanadamu wenzako (Marko 12:30-31). Pamoja na mapungufu ambayo wanadamu wote tunayo, daima kumbuka kwamba upemdo ndicho kitu muhimu siku zote (1 Wakorintho 13:13; Ona pia: The Ten Commandments Reflect Love, Breaking them is Evil na What is the Meaning of Life?).

DHAMBI NA SHERIA YA MUNGU

Biblia inafundisha: “Dhambi ni uasi wa sheria” (1 Yohana 3:4). Yesu alizishika na alizifundisha Amri zote Kumi (Kutoka 20:1-17; Torati 4:13; 10:4). Katika Agano Jipya, Kristo alifundisha juu ya kuzishika Amri kupitia mafundisho mabalimbali (Mfano: Mathayo 5:17-48, 12:12). Yesu aliutimiza unabii kwamba: “ataitukuza sheria na kuifanya iwe sifa” (Isaya 42:21). Wakati wa enzi za Agano Jipya na wakati wote wa kihistoria, Wakristo wa kweli wamejitahidi sana kuitii sheria ya Mungu, ikiwemo kuzishika Amri Kumi. Na hili limetabiriwa kuwa litaendelea hadi nyakati zijazo, sawa na Mtume Yohana alivyoongozwa kutuandikia: “…Watakatifu; hawa ndio wazishikao amri za Mungu na imani yake Yesu” (Ufunuo 14:12).

IMANI, TOBA, KUMPOKEA YESU, KUHESABIWA HAKI, UPATANISHO, NA UBATIZO

Mbali na kuvutwa/kuitwa na Mungu (Yohana 6:44; Mathayo 22:14), hatua ya awali kabisa iliyo wazi katika kuwa Mkristo ni kule kusikia (ambayo pia yaweza kuwa kujisomea si kusikia kupitia masikio tu) kwani “imani huja kwa kusikia, na kusikia huja kwa neno la Mungu” (Warumi 10:17). Kisha huyo asikiaye sharti amwamini Yesu Kristo kwa moyo wake wote “aiamini Njia” ambayo Kristo aliifundisha tuishike kupitia neno la Mungu (Matendo 8:36, 24:14). Hivyo, ni wale tu wawezao kujenga imani kutokana na uelewa sahihi wa neno la Mungu ndio wawezao kufikiriwa kuwa wanastahili kubatizwa kuwa wakristo halisi (ijapokuwa, watoto wadogo wa angalao mzazi Mkristo mmoja, Mungu anawakubali kuwa ni “watakatifu” kulingana na (1 Wakorintho 7:14).

Kuupokea na kuukubali ujumbe wa Yesu hupelekea kwenye “toba kutoka kwenye kazi zilizokufa na kuleta imani kwa Mungu” (Waebrania 6:1; 1 Wakorintho 6:9-11), ubatizo “katika jina la Yesu Kristo kwa ajili ya ondoleo la dhambi” (Matendo 2:38), na “kuwekewa mikono” (Waebrania 6:2; Matendo 8:14-17) hivyo “utapokea kipawa cha Roho Takatifu” (Matendo 2:38).

Wakristo “huhesabiwa haki kwa damu” (Warumi 5:9) na “hupatanishwa kwa Mungu kupitia kifo cha Mwanae, zaidi sana, baada ya kuwa tumepatanishwa, tutaokolewa kwa uzima wake” (Warumi 5:10).

Ubatizo ni kwa maji (ona: Yohana 3:23). Neno la Kigiriki “baptizo” ambako ndiko tumepata neno “batiza” maana yake halisi ni “zamisha, funika ndani ya maji.” Kule kuzamishwa mwili wote kwenye maji wakati wa ubatizo kunasaidia kutoa picha ya mtu aliyejitoa kikamilifu kwa Mungu (Warumi 6:3-13). Agano Jipya laonyesha kuwa Roho Takatifu ilitolewa kwa wale waliokuwa wamebatizwa kupitia kuwekewa mikono na watumishi wa Kristo, kama vile mitume ama wachungaji – wazee wa kanisa (Matendo 8:17; 9:17; 19:6; 2 Timotheo 1:6).

Pale mtu apokeapo Roho Takatifu, Mkristo huyu huwa tayari ametungwa mimba ya ki- Mungu (ona: 1 Petro 1:3; 1 Yohana 5:1), kisha, baadaye huja kipindi cha kukua kiroho/kuatamiwa (ona: 2 Petro 3:18), Wakristo hawa baadaye watazaliwa tena (kwa mara ya pili) kwenye siku ya ufufuo (Yohana 3:5-7) sawa na Kristo alivyozaliwa pale alipofufuka (Warumi 1:4-5).

UUNGU NA WAKRISTO WA KWELI

Wakristo huamini juu ya Baba, Mwana, na Roho Takatifu. Mungu Baba na Mungu Mwana ndio waundao “Uungu” (Warumi 1:20; Wakolosai 2:9). Mungu ni mmoja tu (Marko 12:29; Yohana 17:11; Wakorintho 8:4) na maandiko yanadhihirisha kuwa Mungu ni familia takatifu iishiyo milele ambayo awali imekuwa na wawili, Mungu Baba na Neno ambaye baadaye alifanyika Mwana, (Mwanzo 1:26;  Waefeso 2:19; Yohana 1:1,14), ambapo watoto waaminifu – wakristo wa kweli nao wataongezwa katika familia hii kupitia kutungwa mimba ya Roho Takatifu (Yohana 17:10-11; Waebrania 2:10-11, 1 Yohana 3:1-2; Waefeso 3:14-15). Yesu (ambaye ni Neno na Mwana wa Mungu) pamoja na Baba wote ni Mungu. Roho Takatifu hutoka kwa Mungu (1 Wafalme 8:27; Zaburi 139:7; Yeremia 23:24) na hutolewa kwa wote wanaotubia dhambi zao na kubatizwa (Matendo 2:38-39). Pamoja na kuwa si Mungu mwingine, Roho Takatifu ni nguvu—uweza toka kwa Mungu (Matendo 1:8; 2 Timotheo 1:6-7) ambayo huwasaidia waumini wote waweze kushinda uovu (Warumi 12:21; Ufunuo 2:26-27) na itawaongoza waweze kuufikia uzima wa milele (Wafilipi 3:12; Warumi 6:23). Kuwa nayo “Roho ya Mungu” “Roho ya Kristo” huwatofautisha Wakristo mbali na wale wasio Wakristo (Warumi 8:9). Wengi wadhaniao kuwa ni wakristo, lakini hawashiki sheria, siyo wa Kristo na wala hawakai katika pendo lake (Mathayo 7:21-23; Luka 13:24-27; Yohana 15:9-10; 1 Yohana 2:6).

INJILI YA KRISTO YA UFALME

Injili ya Ufalme ndiyo uliokuwa ujumbe ambao Yesu (Marko 1:14; Luka 4:43; Mathayo 9:35) na wanafunzi wake walihubiri (k.m. Matendo 19:8; 20:25; 28:23; 28:30-31; 2 Petro 1:10-11). Hii “Habari Njema” inahusisha mafundisho juu ya toba, msamaha wa dhambi kupitia sadaka ya Kristo msalabani, upendo na njia ya Mungu ya maisha, na kuhusu Ufalme unaokuja hivi karibuni na serkali ya Mungu (Marko 1:14-15; Matendo 2:38-39; 1 Wakorintho 1:23; 2:2). Injili ya Kristo ya Ufalme wa Mungu inapaswa kwa sasa kuhubiriwa na inafunua njia ambayo kwayo Wakristo watafanyika kuwa washiriki katika kutawala kwenye Ufalme wake (Mathayo 24:14; Matendo 8:12; 17:7; 28:30-31; Ufunuo 2:26-27). “Kuja kwake. Hapo ndipo mwisho utakapokuja, atakapoukabidhi Ufalme kwa Mungu Baba, pale atakapositisha tawala zote na mamlaka zote na nguvu” (Wakorintho 15:23-24).

Hii “Habari Njema” inahusisha ukweli kwamba Mungu hatimaye atatoa wokovu kwa wote (Luka 3:6; Yohana 3:16-17; 12:32,47; Isaya 6:9-11) (What is the Gospel?, The Gospel of the Kingdom of God was the Emphasis of Jesus and the Early Church, na Universal Offer of Salvation: There Are Hundreds of Verses in the Bible Supporting the Doctrine of True Apocatastasis).

Sisi katika Kanisa la Continuing Church of God tunatarajia kuongoza hatua hii ya mwisho ya kazi ya Mungu (the final phase of the work of God) itakayodumu hadi pale Yesu arudipo.

WOKOVU NI KUPITIA JINA LA YESU KWA NEEMA KUPITIA IMANI NA ATAREJEA

“Yesu Kristo wa Nazareti…kwani hakuna jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu ambalo tupaswalo kuokolewa kwalo” (Matendo 4:10, 12). “Yesu akamwambia: “Mimi ndiye njia, kweli na uzima. Mtu haji kwa Baba isipokuwa kwa njia yangu” (Yohana 14:6). “Maana kwa neema mmeokolewa kwa njia ya imani, na hii si kwa uwezo wenu; ni karama ya Mungu, si kwa matendo, mtu asije akajivuna” (Wefeso 2:8-9). Hii ni zawadi ya Mungu kwa neema kupitia imani katika Yesu Kristo (Tito 3:5; 2 Wakorintho 2:15; Warumi 5:10).

Mungu ni mwenye huruma (Kutoka 34:6; Luka 6:36) na anataka wote waweze kuokolewa (I Timotheo 2:4), lakini kutokana na ugumu mbalimbali, ni wachache tu ndio watakaoufikia wokovu katika kipindi hiki (Mathayo 7:14; Luka 13:23-24; Warumi 11:6-7; 2 Wakorintho 4:4). Baada ya kutubu na kubatizwa, Mungu humuhesabia haki Mkristo aliyetubu na hapo ndipo huanza hatua endelevu ya “kuokolewa“ kadri tunavyozidi kukua katika neema na katika kumjua Kristo (2 Petro 3:18) na kuendelea kumruhusu Kristo azidi kuishi ndani yetu (Wagalatia 2:20). Wokovu kwa wale Wakristo wa kipindi cha enzi hizi utakamilika kwenye Siku ya Ufufuo (1 Wakorintho 15:50-54); “Kristo alitolewa mara moja tu azibebe dhambi za wengi. Kwa wale ambao wanamgonjea kwa saburi atatokea kwa mara ya pili, akiwa bila ya dhambi, kwa ajili ya wokovu” (Waebrania 9:28). (Universal Offer of Salvation: There Are Hundreds of Verses in the Bible Supporting the Doctrine of True Apocatastasis na Hope of Salvation: How the Genuine Church of God Differs from Protestantism).

UPENDO NA WOKOVU KWA WANADAMU WOTE NA WA MATAIFA YOTE

Chuki itokanayo na ubaguzi wa rangi ni kosa. Pamoja na uwezekano wa kuwepo tofauti zitokanazo utaifa na rangi, Biblia haifundishi kuwa watu wa rangi fulani ni bora machoni pa Mungu kuliko wengine. Biblia inawaagiza wanadamu wote kila mmoja ampende jirani yake sawa na ajipendavyo mwenyewe (Walawi 19:18; Mathayo 22:39; Matendo 17:24-29). Yesu alikuja kuleta furaha kwa watu wote wa rangi na mataifa yote (Luka 2:10). Biblia inaonyesha kuwa wokovu kwa kipindi hiki unatolewa bure na kwa watu wa asili/rangi zote—wayahudi na watu wa mataifa pia (Matendo 10:34-35; Warumi 10:12-13; Yoeli 2:32) na kwamba Mungu anakusudia kuwaokoa wote wa “kila taifa, kabila, jamaa, na lugha” (Ufunuo 7:9). Upendo wa Kikristo unapaswa uonyeshwe kwa watu wote wa asili zote za binadamu (Warumi 13:10; Luka 10:30-37). “Mungu wetu ni Mungu wa wokovu” (Zaburi 68:20) “Na watu wote wa asili/rangi zote watauona wokovu wa Mungu” (Luka 3:6).

JINA LA KIBIBLIA LA KANISA

Jina mahususi la Kanisa la kweli katika Agano Jipya ni “Kanisa la Mungu.” Mabadiriko juu ya tamko la jina hili  mara kwa mara yametumika ama kuonyesha uwingi ama umoja, yakipatikana katika sehemu tofauti kumi na mbili ndani ya Agano Jipya (Matendo 20:28; 1 Wakorintho 1:2; 10:32; 11:16,22; ;15:9; 2 Wakorintho 1:1; Wagalatia 1:13; 1 Wathesalonike 2:14; 2 Wathesalonike 1:4; 1 Timotheo 3:5,15).  Wakati wote wa historia ya Ukristo, kanisa la kweli limetumia tamko la jina “Kanisa la Mungu” (au Kanisa la Kristo, mfano: Warumi 16:16) japo muda wote pakiongezewa kipengele kingine, kama vile eneo la sehemu lilipo (mfano: 1 Wakorintho 1:2) au hata neno jingine, likiambatana nalo (1 Timotheo 3:15). Yesu alitamka kwamba Wakristo wangelindwa wabaki katika Jina la Baba yake (Yohana 17:12), ambalo siku zote katika Agano Jipya linajulikana kwa ufupi na kwa urahisi kuwa ni “Mungu”, hivyo kanisa liliitwa kuwa ni mali yake, yaani “Kanisa la Mungu”. Kanisa lililo na uaminifu kuliko yote katika Kitabu cha Ufunuo kwa nyakati hizi za mwisho ni lile la Filadefia, lakini kwa kuwa wakati huu ni mabaki tu ya kanisa hili ndio waliosalia, jina “Mabaki ya Filadefia ya Kanisa la Mungu” ndiyo ufafanuzi sahihi wa kundi la Kanisa la Mungu linaloendelea kung’ang’ania kwenye mafundisho ya enzi za Filadefia. Kwa kuwa Kanisa la Mungu limeendelea kuwepo kuanzia enzi za mitume wa awali, basi jina: Continuing Church of God (Kanisa la Mungu Lidumulo) linasaidia kuwakilisha kundi la mabaki yake ya wakati huu.

HISTORIA YA KANISA

Yesu alifundisha kwamba wafuasi wake wa kipindi cha Enzi za Kanisa wangebakia wakiwa “kundi dogo” (Luka 12:32), au kama wanavyotajwa sehemu nyingine kuwa ni “mabaki” sawa na anavyowaita Mtume Paulo (Warumi 11:5). Kanisa la Continuing Church of God kihistoria limetokea kwenye Kanisa la Mitume la Kitabu cha Matendo ambalo ndilo la (Enzi za Efeso), ambalo limepitia enzi mbalimbali hadi leo likiwa katika maeneo mbalimbali. Chakuvutia ni kwamba, Biblia inaonyesha wazi kuwa kanisa la kweli halikubakia kuwa na makao yake makuu katika mji mmoja pekee katika karne zake za kihistoria (Waebrania 13:14; Mathayo 10:23), hivyo, kwa kuuelewa ukweli kuhusu Makanisa saba ya Ufunuo sura ya pili na ya tatu inasaidia kulitambua Kanisa la Mungu la kweli katika maeneo mbalimbali liliko. Ni kanisa la Mungu la kweli, si mji, ndilo litakalodumu kuwepo hadi pale Kristo arudipo (Mathayo 10:23; 16:17-18). Kwa maelezo zaidi, tafadhali jisomee makala yetu The History of Early Christianity (Historia ya Ukristo wa Awali).

SABATO, MILLENNIA, NA SIKU TAKATIFU

Sabato huwadia kila siku ya saba ya juma (Mwanzo 2:2-3; Kutoka 20:8-11; Waebrania 4:4, 9). Biblia yaonyesha kwamba Yesu Kristo (Luka 4:16; 6:6; 13:10; Marko 6:2), Mitume wa awali (Matendo 17:2; 18:4), pamoja na wale waliojitahidi kuwa waaminifu wakati wa mwanzo wa kanisa (Matendo 17:2-4) waliishika amri ya Mungu ya Sabato (Kutoka 20:8-11; Waebrania 4:9). Yesu alijitangaza wazi kwamba yeye ndiye aliyekuwa “Bwana wa Sabato” (Marko 2:28); hivyo katika maana hiyo, “Siku ya Bwana” halisi ni Sabato ambayo hufika kila ifikapo Jumamosi (siku ya saba) ya kila juma. Sabato kwa wakati wote ndiyo imekuwa ishara ya kuwatambulisha Mungu na watu wake (Kutoka 31:13). Likizungumzia juu ya siku ya saba (Waebrania 4:4), Agano Jipya linafundisha kwamba “Imesalia Raha ya Sabato ya mwisho kwa walio watu wa Mungu” (Waebrania 4:9). Hali kadharika, Sabato pia husaidia kama kielelezo cha Utawala wa Kristo wa Millenia (Waebrania 4:1-4; 2 Petro 3:8; Ufunuo 20:4-6).

Biblia inafundisha kwamba Ufalme huu wa Millenia utakuwa ni mzuri ajabu (Isaya 2; 9; 11:1-10; 35:1-9;  Ezekia 34:21-29, Mika 4:1-4; Matendo 3:19-21) na kwmba watakatifu watatawala pamoja na Kristo (Ufunuo 20:4-6).   Shetani Ibilisi ataondolewa na kuwekwa kizuizini wakati huo (Ufunuo 20:1-6), na utakuwa ni wakati wa kupumzika na wenye baraka tele.

Sabato yenyewe hutekelezwa kila juma tangia jua linapozama kwenye siku ya sita ya juma ambayo leo ni Ijumaa hadi jua linapozama tena kesho yake ambapo leo hujulikana kama Jumamosi.

Pamoja na ukweli kwamba baadhi ya taratibu walizotumia zimebadirika ukilinganisha baina ya Enzi za Wana wa Israeli na Enzi hizi za Kanisa, bado ukweli ni kwamba Watakatifu wa awali walizishika Siku Takatifu zote zilizoainishwa katika Maandiko ya Kiebrania kwenye Walawi 23, isipokuwa maana pana zaidi ya Enzi za Agano jipya kuhusu lengo la Sikukuu hizi ndiyo iliongezeka.

Sikukuu ya Pasaka, husaidia kama kielelezo cha mateso na sadaka ya Yesu Kristo ambaye maandiko yanamwonyesha kuwa ndiye alikuja awe “Mwanakondoo wa Mungu aondoaye dhambi ya ulimwengu” (Yohana 1:29). Yesu aliishika Pasaka kila mwaka (Mathayo 26:18; Marko 14:14; Luka 2:41-42; 22:15), akauawa kwenye siku hiyohiyo ya Pasaka (Luka 22:15), na alisurubiwa kwa ajili yetu akiwa ndiye “Kristo, Pasaka wetu, alisurubiwa kwa ajili yetu” (1 Wakorintho 5:7). Yesu alifanya mabadiriko kadhaa juu ya namna ya kuishika Pasaka akiongeza vielelezo vya mikate isiyo na chachu na divai (Mathayo 26:17, 26-28; 1 Wakorintho 11:23-26) pamoja na zoezi la kielelezo cha usafi wa moyo la kuoshana miguu (Yohana 13:1-17).  Pasaka hutimia na kushikwa mara moja kila mwaka (Kutoka 13:10).

Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, ambayo hufuatia kesho yake mara baada ya Pasaka, ni kielelezo cha kusafishika kutoka dhambini kwa kuipokea damu ya sadaka ya Kristo ( 2 Petro 1:9-11). Siku hizi saba za Sikukuu hii zinaainisha pia kwamba chachu ya unafiki, uongo, na uovu wote kwa ujumla sharti iondolewe mbali toka kwa wakristo (Luka 12:1; 1 Wakorintho 5:6-13). Mtume Pauo alivuviwa kutuandikia kwamba: “Hivyo basi na tuifanye Sikukuu (Karamu), si kwa chachu ya kale, wala si kwa chachu ya uongo na uovu, bali kwa mkate usiochachuka wa weupe wa moyo na kweli” (1 Wakorintho 5:8).

Sikukuu ya Pentekoste, ambayo imefafanuliwa katika maandiko ya Kiebrania kama “Sikukuu ya Mavuno, ya malimbuko” (Kutoka 23:16), ni kielelezo cha kuanza kwa kanisa la Agano Jipya (Mwanzo 2:1-4). Pentekoste vilevile inasaidia kuonyesha kwamba Wakristo ni mfano wa mavuno ya awali (Malimbuko) miongoni mwa mavuno yote ya Mungu (Warumi 8:23; 11:16; 1 Wakorintho 15:20-23; Yakobo 1:18), japo “watendakazi ni wachache” (Mathayo 9:37-38). “Hawa ndio wale wamfuatao Mwanakondoo kila aendako. Hawa wamenunuliwa kutoka miongoni mwa wanadamu, ni malimbuko kwa Mungu na kwa Mwanakondoo” (Ufunuo 14:4-5).

Sikukuu ya Kuzipiga Baragumu, inasaidia kutoa kielelezo cha kupulizwa kwa Parapanda Saba katika kitabu cha Ufunuo (Ufunuo 8, 9, 11:15-18), ikiwemo “Parapanda ya Mwisho. Maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa wasiwe na uharibifu, nasi tutabadirika” (1 Wakorintho 15:52).  “Maana Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, pamoja na sauti ya Malaika Mkuu, na parapanda ya Mungu. Nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza” (1 Wathesalonike 4:16).  Kila miaka saba, mwaka wa kuachilia madeni na kupumzisha ardhi huanza kwa kuwadia sikukuu hii (Walawi 25:1-7; Torati 15:7-11).

Sikukuu ya Upatanisho, ambayo hujulikana katika Agano Jipya kama “Mfungo” (Matendo 27:9), husaidia kama kielelezo cha kuonyesha ukweli juu ya udhaifu tulionao na kuhitaji kwetu kudumu karibu na Mungu (Isaya 58:5, 11).  Vilevile inasaidia kuonyesha kuwa Ibilisi Shetani anawajibika na dhambi za wanadamu na kwamba kutokana na hilo, siku hii itakapowadia, atakamatwa na kutiwa kifungoni kwa muda wa miaka elfu moja (Ufunuo 20:1-3; Walawi 16:20-26; Isaya 14:12-16).

Sikukuu ya Vibanda, ambayo ni kielelezo cha wakati wa baraka tele, inasaidia kutuonyesha kuwadia kwa Utawala wa Millenia (Ufunuo 20:4-5) wa Yesu Kristo na Watakatifu utakaoitawala dunia (Zakaria 14; Mathayo 9:37-38; 13:1-30; Luka 12:32; Yohana 7:6-14; Matendo 17:31; Ufunuo 5:10, 12:9). Paradiso hii ijayo, itakayofuata baada ya wanadamu na dunia kukaribia kuangamizwa kabisa kutokana na kazi na mipango mibovu ambayo wanadamu watajisababishia wenyewe ikiwemo pia na Dhiki Kuu na Siku ya Bwana (Mathayo 24:21-31), itasaidia kuwaonyesha wanadamu juu ya faida ya kuishi kwa njia za Mungu za maisha. Kila miaka saba, Sikukuu hii inapowadia, sheria ya Mungui inatakiwa isomwe kwa wanaohudhuria Sikukuu (Torati 31:10-13).

Sikukuu ya Mwisho, husaidia kama kielelezo cha kuonyesha kwamba wanadamu wote waliowahi kuishi bado watapewa fursa yao ya kupata wokovu—fursa ambayo waliowengi wataipokea (Yohana 7:37-39; Warumi 11:25-26; Ezekia 37:11-14; Waebrania 9:27-28). Jina la Agano Jipya la Sikukuu hii limetokana na Mtume Yohana aliyetuandikia, “Siku ile ya mwisho, siku ile kuu ya Sikukuu, Yesu akasimama na kupaza sauti, akisema: “Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe. 38Yeye aniaminiye, kama maandiko yalivyosema, ndani ya moyo wake kutatoka mito ya maji yaliyohai.” (Yohana 7:37-38).

Historia inaonyesha kwamba wafuasi wa mwanzo wa Kristo, akiwemo Polycarp na wengine, waliishika Sabato kwenye siku ya saba ya juma na pia walizishika Sikukuu zote za Kibiblia tulizoziainisha hapa.

Kwa kuzishika sikukuu ambazo Biblia inazitaja, Wakristo watafikia uelewa sahahi na kwa kina juu ya Mpango wa Mungu wa Wokovu, zikiwemo na baadhi ya hatua ambazo wanatakiwa kuzitekeleza katika kuelekea kwenye wokovu.  Sikukuu za Kibiblia zinaonyesha kwamba Kristo ni kweli alisurubiwa (1 Wakorintho 5:7) na Wakristo wanapaswa waishi pasipo kuwa na chachu ya unafiki, uongo, na uovu (Luka 12:1; 1 Wakorintho 5:6-13). Sikukuu za Kibiblia hali kadharika zinasaidia kuonyesha kwamba, pamoja na baadhi wachache wameteuliwa ili waitwe wakati wa Kipindi hiki cha Kanisa (wateule) (Waefeso 1:4-12; Matendo 2:1-47), zipo enzi zinazokuja (matendo 3:21; Mathayo 12:32), na hatima ya wengine wote ambao fursa yao bado haijawadia bado watapewa fursa kwenye Siku Kuu ya Mwisho (Yohana 7:37-38; 12:47-48; Warumi 10:11-21).

ZAKA NA SADAKA

Biblia inafundisha kwamba “Na zaka yote ya ardhi….ni mali ya Bwana” (Walawi 27:30). Wakristo waliokuwa waaminifu walitii na kufuata maelekezo ya Yesu ya kutoa zaka (Mathayo 23:23) na Mtume Paulo juu ya kutoa sadaka (1 Wakorintho 9:1-14). Wakati katika nyakati za Agano la Kale, zaka zililipwa kwa Ukuhani wa Walawi, lakini katika nyakati hizi za Enzi za Kanisa, hili limebadirika na zaka na sadaka hutolewa kwa wale wanaohudumu kama watumishi wa Kristo (Waebrania 7:1-12). Kupitia zaka na sadaka hizi, Wakristo humtumikia Mungu kwa kusaidia kuihubiri Injili kupitia zaka na sadaka zao (1 Wakorintho 9:9), pia zaka hizi huwahudumia watumishi (1 Timotheo 5:17-18), kanisa (2 Wakorintho 9:6-14), husaidia kuandaa Sikukuu Takatifu (Totati 14:22-26; Matendo 18:21), usimamizi wa kazi na mahitaji ya kanisa (1 Wakorintho 12:28; 2 Wakorintho 9:6-14), pamoja na kuwahudumua wahitaji na wenye matatizo (Torati 26:12-15; 2 wakorintho 9:6-14; Wagalatia 2:10).

MAUTI

“Na kama ilivyoamuliwa kwa kila mtu kufa mara moja” (Waebrania 9:27); “maana wote wametenda dhambi …na mshahara wa dhambi ni mauti” (Warumi 3:23; 6:23).

FUFUO TATU NA HUKUMU TATU

“Maana katika Adamu wote wanakufa, kadharika na katika Kristo wote watahuishwa (watafanywa hai). Lakini kila mtu mahala pake: limbuko (Mtangulizi) ni Kristo, baadaye walio wake Kristo hapo atakapokuja” (1 Wakorintho 15:22-23).

Biblia kwa kweli inafundisha kwamba kuna fufuo tatu; soma: Je, wakristo wa Awali Walielewa NIni Juu ya Ufufuo? (What Did Early Christians Understand About the Resurrection?). Ufufuo unaokuja  (wa kwanza kwa wanadamu) ni ule wa watakatifu utakaokuwa pale Kristo atakaporudi (Ufunuo 20:5-6; Yohana 5:28; 1 wathesalonike 4:16), ufufuo wa pili ni kwa wale wengine wote waliobaki (Ufunuo 20:5a,11-12; Mathayo 11:23-24), na wa tatu ni ufufuo wa waovu waliokuwa wameitwa, wakaijua kweli, na kisha kwa makusudi wakaasi na wale waliokufa baada ya kutimiza miaka 100 bila kuyashika maneno ya Mungu wakati wa Utawala wa Kristo (Ufunuo 20:13b-14; Yohana 5:29; Isaya 65:20).

Biblia inajadiri juu ya hukumu angalau tatu. Wakati wa maisha haya, Wakristo wanapitia hukumu (1 Petro 4:17).  Hukumu ya pili ni ile ya wakati wa Hukumu ya Kiti Kikubwa Cheupe (Ufunuo 20:11-12) ambayo itatokea baada ya utawala wa Millenia wa Yesu na Watakatifu wake kumalizika (Ufunuo 20:4-6), na kisha kutakuwa na hukumu ya Mauti na kaburi  (Ufunuo 20:13-14) kwa ajili ya wale ambao majina yao hayakuandikwa katika Kitabu cha Uzima (Ufunuo 20:15).

HATIMA YA WANADAMU

Biblia inaonyesha kwamba Yesu alifanyika mwanadamu (Wafilipi 2:7) ili kwamba wanadamu waweze kufanyika ndugu zake katika familia ya Mungu (Warumi 8:29; Waefeso 3:14-19). Yesu mwenyewe alikuwa akiomba: “Na utukufu ulionipa mimi nimewapa wao, ili wao wawe wamoja nasi sawa na mimi na wewe tulivyo wamoja: Mimi ndani yao, na wewe ndani yangu; ili upate kukamilika katika umoja, na ili ulimwengu upate kujua kuwa wewe ndiye uliyenituma, na umewapenda sawa na jinsi ulivyo nipenda mimi” (Yohana 17:22-23). Makala yenye maelezo ya kina juu ya swala kama hili ni ile isemayo: (Kufanyika Miungu: Je, Kanisa la Awali Lilifundisha kwamba Wakristo watakuwa Mungu?) Deification: Did the Early Church Teach That Christians Would Become God?

Lakini kwa Wakristo walioitwa na ambao watadumu katika imani hadi mwisho wa nyakati, watazawadiwa kwa kupewa nyadhifa katika Ufalme wa Mungu (Yohana 14:1-3; Ufunuo 3:21; 20:4-6), Utawala ambao utakuwa hapahapa duniani (Mathayo 5:5; Ufunuo 2:26-27; 5:10; Danieli 2:44).

DHIKI KUU, KULINDWA, SIKU YA BWANA, NA KURUDI KWA KRISTO

Yesu alifundisha: “Kutakuwa na dhiki kuu, ambayo mfano wake haujawahi kuweko kuanzia kuweko kwa ulimwengu hadi sasa, wala, haitakuwepo tena nyingine baada ya hiyo.  22 Na kama siku hizo zisingalifupishwa, asingeokoka mtu yeyote; lakini kwa ajili ya wateule siku hizo zitafupishwa” (Mathayo 24:21-22). Biblia inaonyesha kwamba Mungu ameahidi kuwalinda Wanafiladefia waaminifu watoke kwenye “saa ya kujaribiwa” (Ufunuo 3:10), lakini hajaahidi hilo kwa Wakristo wote (Ufunuo 12:14-17).

“Siku ya Bwana” ya mwisho itadumu kwa mwaka mmoja (Isaya 34:8) na itatangulia kurudi kwa Yesu Kristo (Ona: Yoeli 2:30-31; Mathayo 24:29-31 ) na kuanza kwa Utawala wa Millenia wa hatua ya Ufalme wa Mungu (Ufunuo 11:15, 20:4; 1 Wathesalonike 4:13-18).

MPINGAKRISTO SIYE MNYAMA ATOKAYE BAHARINI

Biblia inaonyesha kwamba Mpingakristo wa mwisho ni kiongozi wa kidini tofauti na kiongozi wa kisiasa kama wanavyoamini wengi kinyume na aya za maandiko yanayotumia jina “Mpingakristo” (2 Yohana 7, 1 Yohana 2:18, 1 Yohana 2:22, na 1 Yohana 4:3).  Biblia inafundisha wazi “manabii wengi wa uongo wamekwisha kuwako ulimwenguni…hii ndiyo roho ya Mpingakristo” (1 Yohana 4:1, 3) tena kwamba atajaribu kuonyesha kuwa anayo imani ya kweli ya Kikristo (1 Yohana 2:18-22).

Mpingakristo wa mwisho ndiye mnyama wa pembe – mbili wa Ufunuo 13:11-17 ambaye anaitwa “nabii wa uongo” katika Ufunuo 16:13; 19:20; 20:10. Mnyama mwingine wa Ufunuo 13, yaani “mnyama atokaye baharini” wa Ufunuo 13:1-10 ndiye Mfalme wa Kaskazini wa Danieli 11, na pamoja na kwamba atakuwa kinyume na Kristo, ndiye “Mpingakristo ambaye Mtume Yohana alituonya juu yake (Ijapokuwa Yohana anaonya juu yake katika maandiko mengine mengi pia).

SIYO WA ULIMWENGU HUU

Yesu alifundisha: “Ufalme wangu siyo wa ulimwengu huu” (Yohana 18:36). Yohana Mbatizaji alifundisha: “Msidhuru mtu yeyote” (Luka 3:14). Kihistoria, wale wa Kanisa la Mungu wamefahamu kwamba muumini wa kweli kushiriki kwenye kazi za kijeshi ni dhambi. Tangia enzi za vita vya kimapinduzi hadi enzi za vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi kama Marekani hadi zama hizi, baadhi ya nchi kama Marekani zimekuwa na kipengele cha sheria kinachowaruhusu wanakanisa wa Kanisa la Mungu kutoshiriki kwenye vita ama shughuri za mgambo kutokana na dhamira ya imani yao inayowakataza kuua. Wakristo wa mwanzo hawakukubali kushiriki katika maswala yoyote ya kazi za vita ama ugonmvi wa kisiasa wala michezo yenye hatari kwa mwili wa mwanadamu.

Mtume Paulo alifundisha: “tu mabalozi wa Kristo” (2 Wakorintho 5:20; Waefeso 6:20). Mtume Petro alifundisha kwamba watu wa Mungu walikuwa ni: “taifa takatifu, watu walio tunu kwake, ilimpate kutangaza sifa zake aliyewaita mtoke katika ulimwengu huu” (1 Petro 2:9). Biblia hali kadharika inafundisha kwamba ulimwengu huu umedanganywa na Shetani Ibilisi (Ufunuo 12:9) na kwamba watu wa Mungu wanapaswa wajitenge na ulimwengu (Yohana 15:19; 2 Wakorintho 6:14-17; Ufunuo 18:4). Hivyo, kihistoria, Kanisa la Mungu limefundisha daima kwamba waumini wake hawapaswi kushiriki kwenye siasa za nchi wala maswala ya mahakama za kidunia. Hatahivyo, Wakristo wanatarajiwa wawatii viongozi wa serkali na wa jamii (na kuwaombea mara kwa mara, 1 Timotheo 2:1-3; 1 Petro 2:13-17). Vilevile, wakristo wanatakiwa kulipa kodi na tozo zote zinazoagizwa na serkali na taasisi zake (Soma: taxes (Zaka) (Mathayo 22:17-21), lakini pale panapokuwa na kukinzana kwa sheria za nchi, za wanadamu dhidi ya zile za Mungu, “Tunapaswa kumtii Mungu kuliko mamlaka za wanadamu” (Matendo 5:29).

KUKENGEUKA

Kwa vile wasio—wakristo wa kweli siyo sehemu ya wenye imani ya kweli, hawawezi ‘kukengeuka’ katika mantiki ambayo Mtume Paulo aliielezea pale alipoandika katika 2 Wathesalonike 2:3, 1 Timotheo 4:1, hadi kufikia (“kupotoka toka kwenye imani”), na maeneo mengine ya maandiko. Makala inayoweza kufafanua zaidi juu ya hili ni pamoja na: The Falling Away: The Bible and WCG Teachings (Kukengeuka: Mafundisho ya Kibiblia na ya WCG).

NDOA YA KIBIBLIA

Biblia inafundisha kwamba ndoa ya kibiblia ni ile ambayo ni baina ya mtu mme na mtu mke (Marko 10:6-9) na imekusudiwa idumu maisha yao yote (Mathayo 19:3-9; 2 Wakorintho 7:39). Agano Jipya laonyesha kwamba ndoa husaidia kutoa kielelezo cha uhusiano uliopo kiroho baina ya ndoa ya Kristo na Kanisa (Waefeso 5:22-32). Mungu anachukia talaka (Malaki 2:16) na katika Agano Jipya, talaka inaruhusiwa pale maswala fulani machache sana yanapojitokeza (Mathayo 5:31-32, 19:3-9; 1 Wakorintho 7).

Biblia hali kadharika inafundisha: “Wala msiunganishwe na wasioamini kwa jinsi isyosawasawa. Kwa maana kuna uhusiano gani baina ya haki na wasiohaki? Ama pana uhusiano gani baina ya nuru na giza? Na pana mahusiano gani baina ya Kristo na Beliali? Au aaminiye anasehemu gani na yule asiyeamini?” (2 Wakorintho 6:14-16; 7:39), hivyo Kanisa kwa kawaida hupinga ndoa isifungwe baina ya Mkristo wa kweli na asiyeamini.

JUKUMU LA KANISA (MISSION)

Jukumu la Kanisa ni kuihubiri Injili ya Kristo ya Ufalme wa Mungu (Mathayo 24:14) na hii inaonyesha wazi kuwa ni kutekeleza, uhitimishaji wa hatua ya mwisho ya kazi ya Mungu; ona: the final phase of the work (Hatua ya Mwisho ya Kazi ya Mungu).

Hapa tunakuletea majukumu maalum saba ya Kanisa la Continuing Church of God:

1. Kuihubiri Injili ya Ufalme (Mathayo 24:14) pamoja na wokovu kupitia kwa Yesu Kristo (Mathayo 28:19-20; Matendo 4:10, 12; Warumi 1:13).

2. Kuuhubiri ujumbe wa nyakati za mwisho wa maonyo ya kiunabii ya Biblia, ikiwemo kuja kwa Dhiki Kuu, kwa wazao wa Yakobo na wengine waliopo katika kizazi hiki (Angalia: Ezekiea 3 na 33; Mathayo 24:4-51) kadri tunavyojitahidi kuongoza uhitimishwaji wa hatua ya mwisho ya kazi ya Mungu– final phase of the work.

3. Kuuhubiri upendo wa Kifiladefia (Ufunuo 3:7-12; Yakobo 2:8; Yohana 13:35; Waebrania 13:1), kuwalisha kondoo (Mathayo 28:19-20), na kuwatia moyo wote waweze kufaulu kujenga tabia kwa kuimarika katika neema na elimu ya kumjua Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo (2 Petro 3:18).

4. Kuwa mfano (Mathayo 5:14-16; 1 Wathesalonike 1:7) na kuwa mashahidi (Mathayo 24:14) kwa ulimwengu kwa ujumla, pamoja na kwa wakristo kwa ujumla.

5. Kujifunza na kutekeleza maneno na maagizo ya Yesu katika maisha yetu ya kila siku kwa wengine (Yohana 13:35; 15:14).

6. Kuurejesha ukweli zaidi wa elimu ya Neno la Mungu uliopotea toka kwa Ukristo wa asili (Yuda 3; Mathayo 17:11).

7. Kufundisha kwamba Wakristo wanapaswa kuongozwa na Roho Takatifu na kujitahidi kuwa na upendo, huruma, hukumu za haki, imani, haki pamoja na karama zingine za Roho (1Wakorintho 13:1-14:1; Mathayo 23:23; Wagalatia 5:22-25).

Kuufundisha ukweli na upendo wa neno la Mungu kwa ulimwengu kwa ujumla na hasahasa kwa wale walioitwa katika kizazi hiki (Mathayo 28:19-20) ndilo jukumu la Kanisa la Continuing Church of God.

www.ccog.org

Anwani na Habari zingine Mawasiliano

Kuendelea Kanisa la Mungu (Continuing Church of God) 1036 W. Grand Avenue, Grover Beach, CA 93433  USA

1 (805) 574-1818

 

Posted in African Booklets, Kiswahili, Uncategorized
About CCOG
The Continuing Church of God, which attempts to represent the most faithful remnant of the Philadelphia (Revelation 3:7) portion of the Church of God, bases its beliefs on the Holy Bible. Read CCOG's statement of beliefs for more information.